Posts

Showing posts from January 12, 2018

WAKAZI WILAYANI MPANDA SERIKALI IWAJIBIKE KUTENGA MAENEO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA

Baadhi ya wakazi wa kata ya Magamba Manispa ya Mpanda mkoani Katavi wameitaka serikali kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima ili kuepusha migogoro ya ardhi inayojitokeza mara kwa mara Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema wakulima na wafugaji wanapoendesha shughuli zao katika eneo moja huchangia mifarakano isiyo ya lazima na kushauri wafugaji kutengewa eneo tofauti na wakulima ili kuondoa mwingiliano Kwa upande wake Bi.Anna Thomas ambaye ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Magamba amekiri kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara baina ya wakulima na wafugaji na kuongeza kuwa inachangangiwa na wafugaji kuwa na mifugo mengi kwenye eneo dogo Philemone Tesha Afisa kilimo wa kata ya magamba amesema serikali ina mpango wa kutenga maeneo ya kuchungia yatakayokuwa tofauti na mashamba japo hakubainisha wazi mpango huo ni lini utaanza kutekelezwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MWENYEKITI WA BAVICHA TAIFA ZIARANI KATAVI ATOA NENO

Image
Mwenyekiti wa Taifa   balaza la wanawake la Chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema   Ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee amezitaka taasisi za ndani ya chama hicho kuwajibika vyema katika kukijenga chama hicho. Akizungumza na wanawake wa chama hicho pamoja na vijana katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria  manispaa ya Mpanda  amesema  Taasisi hizo kwa kushilikiana na vijana vinamchango mkubwa katika kukijenga chama hicho Hapa nchini Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu wa chama hicho katika Mkoa wa Katavi Rhoda Kunchela amesema kunavikundi mbalimbali vya akina ambavyo vimeanza kunufaika. Ziara hiyo ya mwenyekiti wa Bawacha Taifa inalengo la  kukagua uhai wa jumuia hiyo na chama kwa ujumla katika mikoa ya Rukwa Tabora na  Katavi  ugeni huo umeambatana na katibu mkuu wa balaza la wanawake la chama hicho Taifa Grace Tendega. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

DK.SHEIN ATUNUKU NISHANI ZILIZOTUKUKA 43

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohammed Shein ametunuku nishani zilizotukuka 43 kwa viongozi na watumishi wa umma ikiwa ni maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Dkt.Shein ametoa nishani hizo kwa mutu ambae aliasisi,alishiriki na kutukuza pamoja na kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar yaliyotokea mwaka 1964. Pamoja na hayo Dk. Shein amewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo ili kuwa chachu ya kuendelea kuwa kivutio kikubwa kwa uwekezaji miradi mikubwa ya maendeleo visiwani . Katika maadhimisho hayo mbali ya nishani hizo serikali ya Zanzibar huzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni ishara ya ukombozi wa fikra na maendeleo ya kiuchumi ya taifa hilo. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

NAIBU WAZIRI ATAKA WATOTO HAPA NCHINI WALINDWE NA KUPATIWA HAKI ZAO MANISPAA YA MPANDA NAO WAJA NA MKAKATI

Image
Na.Issack Gerald Naibu waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile amewataka watanzania kuhakikisha watoto wote wanapatiwa haki zote za msingi katika maisha yao ikiwemo haki za kuishi na kulindwa. Naibu waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile Dkt.Ndugulile ametoa wito huo jana Mjini Mpanda wakati akizungumza na Makundi mbalimbali ya wananchi ambayo yamepewa jukumu la kuelimisha jamii kuhusu haki za mtoto na kuwaibua watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi. Aidha DK.Ndugulile amesema serikali itaendelea kushirikiana na Shirika la JSI la Marekani linalojihusisha na masuala ya jamii ikiwemo kudhibiti mambo yanayomkatisha mtoto kutimiza ndoto zake hasa kielimu. Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Mpanda Bi.Redgunda Mayorwa amesema ushirikiano kati ya serikali na wadau mbalimbali ndiyo njia pekee itakayomukoa mtoto dhidi ya mazngira hatarishi ikiwa ni pamoja na wanai

RAIS KAGAME KUWASILI NCHINI KESHOKUTWA

Image
Rais wa Rwanda Paul Kagame anatarajia kuwasili hapa nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi. Kwa mjibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda Mhe.Paul Kagame anayetarajiwa kuwasili nchini Jumapili ya wiki hii. Makonda amesema hayo leo akiwa katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam baada ya kuagana na Rais Magufuli aliyeelekea visiwani Zanzibar kushiriki sherehe za maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mbali na hilo Makonda amesema kuwa Rais Paul Kagame atawasili nchini Tanzania siku ya Jumapili ya tarehe 14 ambapo atakuwa nchini kwa ziara ya siku moja na kufanya mazungumzo na Rais John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

DKT.SHEIN ATOA MSAMAHA KWA WANAFUNZI 12 WANAOTUMIKIA CHUO CHA MAFUNZO ZANZIBAR

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa msamaha kwa wanafunzi 12 waliokuwa wakiendelea kutumikia vyuo vya Mafunzo vya Unguja na Pemba ikiwa ni miongoni mwa Sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee amsema Rais amechukua hatua hiyo kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 59 cha Katiba ya Zanzibar 1984. Mh.Rais ameamuru kuwa kifungo kilichobaki cha wanafunzi walionufaika na msamaha huo ambao bado wanaendelea kutumikia katika vyuo vya Mafunzo vya Unguja na Pemba kuwa kipindi hicho chote kinafutwa na kwamba wanafunzi hao waachiwe huru kuanzia siku ya jana. Taarifa hiyo imeeleza kuwa Zanzibar inasherehekea miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar 12 Januari 2018 na kwa kuwa Mhe.Rais ameridhika kuwa kuna sababu za kutosha za kutumia uwezo wake huo katika sherehe hii wanafunzi hao waachiwe huru. Walionufaika na msamaha huo kwa U

MANISPAA YA MPANDA KUNUNUA GARI JIPYA LA KUZOA TAKA NDANI YA MWEZI JANUARI MWAKA 2018

Image
Na.Issack Gerald Halamshauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imesema inatarajia kununua gari jipya la kuzoa taka kabla ya mwezi Januari mwaka huu kukamilika. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo Michael Nzyungu ambapo amesema gari hilo lenye ujazo wa tani 16 litagharimu kiasi cha shilingi milioni 160. Aidha Nzyungu amesema halmashauri inaendelea kukarabati magari ya kuzoa taka yaliyopo huku ikiendelea kusubiri gari lingine aliloliahidi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofanya ziara mkoani Katavi mwaka uliopita. Hatua ya ununuzi wa gari jipya ni kufuatia kukithiri kwa taka katika maeneo mbalimbali ya Manispaa hali inayosababisha wakazi kulalamika huku wakihofia mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED