MANISPAA YA MPANDA KUNUNUA GARI JIPYA LA KUZOA TAKA NDANI YA MWEZI JANUARI MWAKA 2018

Na.Issack Gerald

Halamshauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imesema inatarajia kununua gari jipya la kuzoa taka kabla ya mwezi Januari mwaka huu kukamilika.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo Michael Nzyungu ambapo amesema gari hilo lenye ujazo wa tani 16 litagharimu kiasi cha shilingi milioni 160.

Aidha Nzyungu amesema halmashauri inaendelea kukarabati magari ya kuzoa taka yaliyopo huku ikiendelea kusubiri gari lingine aliloliahidi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofanya ziara mkoani Katavi mwaka uliopita.

Hatua ya ununuzi wa gari jipya ni kufuatia kukithiri kwa taka katika maeneo mbalimbali ya Manispaa hali inayosababisha wakazi kulalamika huku wakihofia mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu.


Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA