Posts

Showing posts from March 19, 2018

WATOTO PASUA VICHWA SUMBAWANGA

Image
BARAZA la madiwani la halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa limeviomba vyombo vya usalama vishirikiane na idara ya uhamiaji  kuwakamata na kuwarudisha nchini kwao watoto wa nchi jirani za Zambia na  Congo DRC wanaoishi katika mazingira magumu. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Justine Malisawa alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akiongoza kikao cha baraza hilo baada ya wajumbe kulalamikia kuongezeka kwa watoto ambao wamekuwa kero na kujihusisha vitendo vya uporaji wa mali za raia pamoja na ubakaji. Mmoja wa madiwani hao Vitalis Ulaya alisema watoto hao wanazidi kuongezeka kila kukicha katika mji wa Sumbawanga hali ambayo ni hatari kwa kuwa hakuna jitihada za kutosha za kuweza kukabiliana na wimbi la ongezeko hilo. Alisema kuwa wengi wa watoto hao wanazurula nyakati za mchana  wakiokota vitu majalalani na kuomba hela kwa wapita njia na nyakati za usiku wamekuwa wakifanya vitendo vya uhalifu hali inayosababisha amani kutoweka. Kwa upande wake Ester Mpelel

RAIS MAGUFULI KUKUTANA NA WAWEKEZAJI MABILIONEA WA UJERUMANI NA DENIMARK

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.John Magufuli amesema siku za hivi karibuni anatarajia kukutana na Wakurugenzi Watendaji wawili kutoka nchi za Ujerumani na Demark watakaokuja kufanya uwekezaji nchini. Kauli hiyo ameitoa leo Machi 19,2018 wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara,ambao ulikuwa umebeba maudhui ya ‘Tanzania ya Viwanda na Ushiriki wa sekta binafsi nchini.’ Rais Magufuli amesema watakuja kufanya uwekezaji wa kiwanda kipya cha Petroli Kemikali (Petrol Chemical Plant) ambacho kitakuwa na thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.92 ambayo ni sawa na takriban Shilingi za Kitanzania Trilioni 4.56. Ameeleza kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 4000 katika eneo la Kilwa kwa ajili ya kutengeneza mbolea ambayo itauzwa ndani pamoja na nje ya nchi kwa kutumia gesi iliyopo nchini. Wakati huo huo,amewataka wawekezaji waliopo hapa nchini kutumia fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini kwa kuwa rasilimali zipo za kutosha huku a

JAJI MKUU WA TANZANIA ATOA WARAKA MZITO KWA MAHAKAMA MKOANI KATAVI

Image
Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Khamisi Juma ametoa waraka kwa Mahakama ya hakimu mkazi  Mkoa wa Katavi unaokataza Tozo ya malipo kwa hati za  hukumu ambazo ilikuwa inatozwa kwa wananchi . Jaji mkuu wa Tanzania  Profesa Ibrahim Khamisi Juma Kwa mjibu wa Afisa mawasiliano na Tehama wa mahakama hiyo Jemes Vedasi Kapele amesema waraka huo unaelekeza usitishwaji wa tozo za hati za hukumu. Aidha Afisa huyo   amesema kufutwa kwa tozo hizo kutakuwa mkombozi kwa wananchi wengi wenye kipato cha chini kwani walikuwa wakishindwa kumudu gharama zinazotakiwa kutokana na ukosefu wa fedha wanapohitaji kuapitwa haki zao kwa mjibu wa sheria. Mara kadhaa baadhi ya wananchi wamekuwa wakionekana kutumia baadhi ya aseti kama ardhi ili kugharimia gharama zinazohitajika. Jaji mkuu ametoa waraka huo ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kufanya ziara mkoani Katavi na kutoa kauli ya kufuta tozo hizo. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 1.3 ZA MADAI YA WALIMU MKOANI KATAVI HAWAJANUSA

Image
Chama Cha walimu Tanzania CWT Mkoani Katavi kimesema madai mbalimbali ambayo walimu wanaidai serikali mpaka sasa hayajalipwa. Hatua hiyo imethibitishwa na Katibu wa chama hicho Mkoani Katavi Hamis Ismail Chinahova wakati akizungumzia kuhusu hatua iliyofikiwa ya kulipwa kwa madeni ya walimu. Aidha amesema kiasi cha cha shilingi bilioni 1.3 ambacho walimu Mkoani Katavi wanaidai serikali kinahusu madai ya likizo,uhamisho,matibabu,masomo na stahiki nyingine muhimu ukiondoa suala la mishahara. Kwa mjibu wa taarifa ya iliyokuwa imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango hivi karibuni,takwimu ya madeni ya watumishi nchini inaonesha ni  zaidi ya shilingi bilioni 127 kati ya hizo walimu wakidai shilingi bilioni 16.25 zilizotakiwa kulipwa pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com