Posts

Showing posts from November 3, 2017

ASILIMIA 90 YA WACHIMBAJI MADINI MKOANI KATAVI WANACHIMBA MADINI BILA UTAFITI

Na.Issack Gerald-Katavi Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Magharibi Mhandisi Juma Haruna Sementa,amesema asilimia 90 ya wachimbaji wa madini Mkoani Katavi,wanashindwa kufikia malengo katika uchimbaji madini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutofanya utafiti kabla ya kuchimba. Mhandisi Sementa amesema hayo wakati akizungumzia kuhusu baadhi maeneo ya uchimbaji kutelekezwa ikiwemo maeneo ya Kapalamsenga. Ametaja sababu nyingine inayokwamisha uchimbaji endelevu wa madini mkoani Katavi kuwa ni ukosefu wa mtaji wa fedha za kuendeshea mitambo. Katika hatua nyingine Kamishna Sementa amesema ujenzi wa kituo cha mfano cha kuchenjua madini kilichokuwa kimepangwa kukamilika ujenzi wake mwezi Septemba mwaka huu katika machimbo ya Kapanda,bado haujatekelezwa kutokana na uhaba wa fedha. Hata hivyo ametaja shughuli za uchimbaji madini bila utafiti ndiyo chanzo kinachopelekea uharibifu wa mazingira. Baadhi ya maeneo yanayotajwa kuwa na madini hususani dhahabu Mkoani Katavi ni pamo

WATAKAOKAIDI KUONDOKA KATIKA HIFADHI ZA MISITU WILAYANI MPANDA KUONDOLEWA KWA NGUVU

Na.Issack Gerald-Mpanda Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga amepiga marufu kufanya shughuli za kilimo katika misitu iliyo hifadhiwa akisema kuwa wanaokaidi na kuendelea kuvamia maeneo ya hifadhi wataondolewa kwa nguvu. Bi.Matinga ametoa marufuku hiyo leo wakati akieleza za kuwepo kwa tetesi za baadhi ya wananchi walioondolewa katika maeneo ya hifadhi kutaka kuendesha  shughuli za kilimo. Aidha amesema serikali haitakubali kuangamiza uoto wa asili kutokana na watu wanaovamia misitu kwa kisingizio cha kukosa maeneo ya makazi huku sheria za kupata ardhi kwa matumizi ya kibinadamu zikiwa wazi. Miongoni mwa maeneo yaliyokumbuwa na operesheni ya wananchi  kuondolewa kinguvu  kwa madai ya kuvamia misitu ni Kijiji cha Mgolokani  kata ya Stalike,Kijiji cha Nsanda kilichopo kata ya Katumba na maeneo mengine.                                         Habari zaidi na P5TANZANIA LIMITED