WATAKAOKAIDI KUONDOKA KATIKA HIFADHI ZA MISITU WILAYANI MPANDA KUONDOLEWA KWA NGUVU

Na.Issack Gerald-Mpanda

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga amepiga marufu kufanya shughuli za kilimo katika misitu iliyo hifadhiwa akisema kuwa wanaokaidi na kuendelea kuvamia maeneo ya hifadhi wataondolewa kwa nguvu.

Bi.Matinga ametoa marufuku hiyo leo wakati akieleza za kuwepo kwa tetesi za baadhi ya wananchi walioondolewa katika maeneo ya hifadhi kutaka kuendesha  shughuli za kilimo.

Aidha amesema serikali haitakubali kuangamiza uoto wa asili kutokana na watu wanaovamia misitu kwa kisingizio cha kukosa maeneo ya makazi huku sheria za kupata ardhi kwa matumizi ya kibinadamu zikiwa wazi.

Miongoni mwa maeneo yaliyokumbuwa na operesheni ya wananchi  kuondolewa kinguvu  kwa madai ya kuvamia misitu ni Kijiji cha Mgolokani  kata ya Stalike,Kijiji cha Nsanda kilichopo kata ya Katumba na maeneo mengine.


                                       Habari zaidi na P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA