Posts

Showing posts from December 27, 2017

RAIS MAGUFULI,KENYATTA,NKURUNZIZA,IDRISI,MAHAKAMA YA KENYA NA JSEHI LA ZIMBABWE WATUNUKIWA TUZO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii. Rais Magufuli mwenye miwani katika picha Marais wengine ambao wamepata tuzo ni Rais Uhuru Kenyatta ambaye amejishindia tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya. Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao. Rais wa Taasisi ya Mandela,Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka. Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi. Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi

WATUMISHI WA HOSPITALI MKOANI KATAVI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA YUMO MWANANCHI ALIYESAHWISHI KUTOA SHILINGI 500

Image
Na.Issack Gerald-Katavi TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa ( Takukuru) Mkoani Katavi imewafikisha katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Katavi watuhumiwa watatu  wakiwemo  watumishi wawili wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa. Kwa Mjibu wa taarifa ya Mkuu wa Takukuru Mkoani Katavi John Minyenya kwa vyombo vya habari,amewataja wauguzi wa Hospitali hiyo waliofikishwa mahakamani kuwa ni Yohana Paul Deo(25) mkazi wa Kawajense anayetuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 40,000 kutoka kwa mwananchi aliyekuwa akimuuguza mgonjwa wake baada ya kupata ajali ya pikipiki na kuvunjika mguu na mkono. Deo katika kesi hii,anadaiwa kuomba fedha hiyo Septemba 22 mwaka huu ili amsaidie ndugu wa mgonjwa huyo kupatiwa huduma baada ya kukaa siku mbili hospitalini hapo bila kuhudumiwa. Muuguzi mwingine ambaye amefikishwa mahakamani ni Marco Bunduki James(31) mkazi wa Kawajense ambaye ameshtakiwa kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 30,

JESHI LA POLISI ZANZIBAR LAAMUA KUJITATHMIN

Image
Jeshi la Polisi Zanzibar,limeamua kujitathmini kwa lengo la kusahihisha kasoro watakazobaini ili kutoa huduma bora kwa jamii. Mpango huo wa kujitathmini unafanyika kwa utaratibu wa kusikiliza maoni na ushauri kutoka kwa wananchi,wakilenga zaidi kujenga imani ya raia kwa jeshi hilo. Utaratibu huo wa kujitathmini ulitangazwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Unguja,Makarani Khamis Ahmed kuwa wameamua kufanya hivyo kwa lengo la kuliweka jeshi karibu na jamii na kufanya kazi pamoja ya kupambana na vitendo uhalifu. Huu ni utaratibu mzuri wa kufanya mawasiliano na raia ambao unafaa kuendelezwa kwa maeneo yote ya visiwa vya Unguja na Pemba ambapo imeelezwa kuwa utaratibu huu utaondoa au kupunguza kwa kiasi kikubwa uadui au hofu iliyojengeka kati ya raia na polisi. Aidha ni nafasi nzuri kwa maofisa wa Jeshi la Polisi kuwaelimisha raia na kuwaeleza dosari wanazoziona katika jamii katika kupambana na vitendo vya uhaifu na kuwatia hatiani wanaofanya vitendo hivyo. Chanzo:Zanzibar

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU KUZIMWA KWA 'CHANELI' ZA BURE KWENYE VING'AMUZI

Image
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas amesema, kwa mujibu wa sheria iliyopo sasa vituo vyote vya runinga ambavyo vimepewa leseni ya FTA (Free to Air) vinapaswa kuonekana hata baada ya kifurushi kwenye kisimbusi kwisha. Dkt.Hassan Abbas Ufafanuzi huu unatolewa kufuatia uwepo wa malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wananchi kuhusu kukosa huduma ya runinga za bure pindi vifurushi katika visimbusi (ving’amuzi) vyao vinapomalizika Dkt.Abbas amesema hadi sasa kuna vituo 16 vya runinga vya ndani ya nchi vilivyopewa leseni hizo vikiwemo vituo vya ITV,Clouds TV na Channel 10. Amesema ili mtumiaji atazame Runinga hata baada ya kufurushi chake cha malipo kwisha,kituo cha runinga (mfano ITV) kinapaswa kuwalipa warushaji wa masafa (mfano Azam) ili ITV iweze kuonekana kwa wananchi hata ambao hawajalipia visimbusi vyao. Wakati huo huo Dkt.Abbas ametahadharisha kuwa, endapo kituo cha runinga hakitawalipa wasafirishaji wa masafa watakatiwa huduma na hivyo kuwafanya wananchi washindw

MAREKANI YAWAWEKEA VIKWAZO WATAALAMU WA MAKOMBORA KOREA KASKAZINI

Image
Marekani imewawekea vikwazo maafisa wawili wa Korea Kaskazini akidai wamechangia kuundwa makombora ya nchi hiyo. Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol Wizara ya fedha nchini Marekani iliwataja Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol na kusema kuwa wote walikuwa viongozi wakuu katika mpango wa makombora ya masafa marefu wa Korea Kaskazini. Baraza la ulinzi la Umoja wa Mataifa liliiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini siku ya Ijumaa kujibu majaribio yake ya makombora ya masafa marefu huku Korea Kaskazini ikisema kwa hatua hiyo ni kama ya vita. Vikwazo hivyo vipya vya Marekani vitazuia shughuli zozote za wanaume hao wawili zinazofanywa nchini Marekani na hata kutwaliwa kwa mali yao zilizo nchini Marekani. Wanaume hao wawili wanaonekana mara kwa mara wakiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wakiwa maeneo ya kuyafanyia majaribio makombora. Mwaka huu nchi hiyo imefanya majaribio kadha ya makombora tofauti ambayo Korea Kaskazini i nasema y