Posts

Showing posts from January 27, 2018

MAJAMBAZI WAUA MMOJA KATAVI,WAJERUHI WENGINE NA KUPORA FEDHA

Na.Issack Gerald Mtu mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jina la Hassan Damsoni mkazi wa kijiji cha Katambike kata ya Ugalla Mkoani Katavi ameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi. Kwa mjibu wa diwani wa kata hiyo Mh.Halawa Malembeja amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa tano usiku ambapo mbali na kuuwawa kwa makzi huyo watu hao wamepora zaidi ya shilingi milioni mbili kutoka nyumba tano na kujeruhi wengine. Kwa mjibu wa Diwani Malembeja mazishi ya marehemu yamekwishafanyika katika kijiji hicho huku akieleza kuwa wananchi wamesikitishwa na tukio hilo na kuliomba jeshi la polisi kupeleka kituo cha polisi katika kata hiyo kwa ajili ya usalama. Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda amekiri kutokea kwa tukio hilo na amesema wamemkamata mtu mmoja akiwa na silaha aina ya gobole na simu tano ambazo zilikuwa zimeondolewa. Hata hiyo Jeshi la polisi limetoa wito kwa watu kuacha kujihusisha na uharifu kwani kufanya hivyo ni

WAWILI WAUWAWA KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI KATAVI

Image
Na.Issack Gerald Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limewauwa watu wawili kati ya watano waliokuwa na silaha tatu za kivita aina ya SMG ambapo watu hao wameuawa wakati wa majibizano kati yao na Jeshi la Polisi. Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda amesema tukio hilo limetokea Januari 25 mwaka huu katika kijiji cha Kapalamsenga Wilayani Tanganyika ambapo watu hao wamekutwa wakiwa na risasi 16 na Magazini 5. Aidha Kamanda Nyanda amesema watu hao wamekutwa na meno ya Tembo yenye uzito wa kilo 6.6 yakiwa na thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 34  pamoja na nyama ya pofu kilo 20 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3 Kwa upande wake Mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Katavi Zumbe Msindai amesema kukamatwa kwa watu hao kumetokana na ushirikiano kati yao na jeshi Polisi Mkoani Katavi ikiwa ni baada ya kupata taarifa za siri juu ya uwepo wa watu hao. Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR KUSHIRIKIANA NA MSD KATIKA UAGIZAJI DAWA NA VIFAA TIBA

Image
WIZARA   ya Afya Zanzibar imetiliana saini makubaliano ya ushirikiano na Bohari ya Dawa Tanzania (msd) katika masuala ya uagiziaji dawa na vifaa Tiba kutoka viwandani moja kwa moja na hatua hiyo itaiwezesha Zanzibar kupunguza gharama kubwa ya kuagiza dawa kutoka katika makampuni. Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla Juma alitia saini kwa upande wa Wizara hiyo na Mkurugenzi   Mkuu Laurean Rugambwa Bwanakunu aliiwakilisha Bohari kuu ya Dawa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Zanzibari Mnazimmoja. Akizungumza baada ya kutiliana sani Bi. Asha Abdalla alisema ushirikiano huo utaisaidia Serikali na wananchi kwa ujumla kuwa na uhakika wa upatikanaji dawa na kupunguza mzigo wa kutumia gharama kubwa kuagiza dawa. Alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhakikisha   dawa zote zinapatikana   bila usumbufu katika Hospitali na vituo vya afya na kufanikisha   malengo yake ya kuwapatia wananchi   huduma bora za afya. Katibu Mkuu Wizara ya Afya ame

HAKIMU ATAKA WATENDAJI WA MAHAKAMA WAWAJIBIKE KWA MJIBU WA SHERIA

Image
Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Katavi Hassan Omary amewataka watendaji wa mahakama kusimamia maadili ya kazi zao katika uwajibikaji wa kuwatumikia wananchi katika kutoa maamuzi mbalimbali ya kesi wanazoziendesha ktika maeneo yao yakazi. Bw.Omary amesema kuna baadhi ya malalamiko ambayo amekuwa akiyapokea kutoka kwa wananchi yanayowalenga moja kwa moja baadhi ya watumishi wa mahakama katika utekelezaji wa majukumu yao kwa wananchi hasa yale ya ucheleweshwaji wa maauzi ya kesi pasipo na sababu za msingi Aidha amesisitiza kuwa nivyema wanachi kufahamu kuwa mahakama ndiyo sehemu sahihi ya kukimbilia pindi wanapoona haki zao zinapolwa na watu wasio jua taratibu kanuni na sheria za nchi pamoja na hayo amesema muhimili huo wa utoaji haki nivyema ukaachwa ufanyekazi yake pasipokuingiliwa na Mtu au taasisi yeyote katika utoaji wa maamuzi mbalimbali ya kesi Kwa upande wake afisa Tehama wa mahakama hiyo Bw.James Kapele amesma kuwepo kwa mfumo wa kieletroniki katika undeshaji wa kes

HALMASHAURI YATOA TAHADHARI KWA WAZAZI KUPELEKA WATOTO KATIKA SHULE ZISIZOSAJILIWA

Na.Issack Gerald Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imetoa tahadhari kwa wazazi Mkoani Katavi wanaowapeleka watoto wao katika shule mbalimbali za Manispaa ambazo hazijasajiliwa. Kauli hiyo imetolewa na Afisa elimu taaluma Manispaa ya Mpanda Mwalimu Rashid Pili wakati akizungumza kuhusu uwepo wa baadhi ya shule ambazo hazijasajiliwa lakini tayari zikiwa zimesajili wanafunzi wa shule za msingi na chekechea. Kwa mjibu wa Mwalimu Pili,Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ina Shule 36 zikiwemo 34 za serikali na 2 za binafsi za Reimeta na Nzela English Pre-Primary School zinazotambuliwa na serikali ambapo mtoto anayesajiliwa nje ya shule hizo hatambuliki katika mfumo wa elimu Tanzania. Hata hivyo Mwalimu Pili amesema Ijumaa ya Wiki hii wanatarajia kukutana na wamiliki wa shule hizo ili kufikia mwafaka ili kuendesha mambo kwa kufuata misingi ya sheria na kanuni za nchi. Aidha Mwalimu Pili amesema katika mwaka 2018 manispaa ya Mpanda imejipanga kufaulisha kwa karibu asil

KENYATTA ATEUA MAWAZIRI WAPYA KENYA NA BALOZI MPYA TANZANIA

Image
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe kuwa mawaziri katika serikali yake mpya baada yake kushinda uchaguzi mwaka jana. Rais Uhuru Kenyatta Mawaziri sita ambao walikuwa wanahudumu katika serikali yake muhula uliopita wamevuliwa uwaziri na kuteuliwa kuwa mabalozi. Bw.Dan Kazungu ambaye amekuwa waziri wa madini, amependekezwa kuwa balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania. Aliyekuwa balozi wa Kenya nchini humo Chirau Ali Mwakwere alijiuzulu mwaka jana ili kuwania kiti cha ugavana katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti. Miongoni mwa walioteuliwa kuwa mawaziri wapya ni mwanahabari mkongwe Farida Karoney ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa ardhi. Wadhifa huo ulikuwa unashikiliwa na Prof Jacob Kaimenyi ambaye amependekezwa kuwa balozi wa Kenya katika Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Sayansi, Elimu na Utamaduni (Unesco) mjini Geneva. Bi.Monica Juma ameteuliwa kuwa waziri mpya wa mambo ya nje kuchukua nafasi ya Amina Mohamed ambaye amependekez

ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TBC AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTAPANYA SHILINGI MIL. 897

Image
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Tido Mhando amefikishwa mahakamani jijini Dar es Salaam kwa mashtaka ya matumizi mabaya ya Madaraka. Tido Mhando Tido Mhando,ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media alifikishwa katika mahakama ya Kisutu mapema jana Ijumaa na kusomewa dhidi mashtaka yake. Wakili wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) Leonard Swai alimwaambia hakimu mkazi mkuu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Victoria Nongwa kuwa Mhando anatuhumiwa kwa mashtaka matano. Bw.Mhando anadaiwa kutenda makosa hayo mwaka 2008 alipokuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC na anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka wakati alipokuwa akilitumikia shirika hilo la Utangazaji la Serikali TBC ambapo anadaiwa kulitia hasara taifa shilingi milioni 897. Hata hivyo Mhando amekana mashtaka yote na kuachiwa kwa dhamana ambapo kesi imeahirishwa hadi Februari 23mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali. Sheria nchini Tanzania haiwaruhusu washtakiwa,mawa

DIWANI ATAKA MKURUGENZI ATAFUTE MAENEO KWA AJILI YA WAPIGA KURA WAKE

Diwani wa Kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Mh.Willium Liwali amemshauri Mkurugenzi mtendaji Manispaa ya Mpanda kutafuta mahali pa kuwaweka wafanyabiashara wadodo wadogo wapatao 200 wa kata hiyo waliokosa nafasi ya kufanyia biashara. Mh.Liwali amesema hayo kufuatia agizo la Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu kuagiza wafanyabiashara wote walio katika masoko yasiyo rasmi katika Manispaa hiyo kutakiwa kuondoka na kufanyia biashara zao katika masoko rasmi. Kwa mjibu wa Diwani Liwali masoko yote ambayo wafanyabiashara hao wangehamia yakiwemo soko la Mpanda Hotel lililopo kata ya Majengo na soko la Kachoma lililopo kata ya Makanyagio yote yamejaa. Wiki iliyopita,mamia ya wafanyabiashara wadogowadogo wanaofanyia biashara zao katika machinjio ya ng’ombe Mpanda Hotel waliandamana mpaka kituo cha Radio Mpanda Fm wakipinga agizo la Mkurugenzi anayewataka kuondoka katika maeneo hayo yasiyo rasmi. Kwa mjibu wa agizo la Mkurugenzi Michael Nzyungu,wafanyab

DIWANI ATAKA MKURUGENZI ATAFUTE MAENEO KWA AJILI YA WAPIGA KURA WAKE

Diwani wa Kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Mh.Willium Liwali amemshauri Mkurugenzi mtendaji Manispaa ya Mpanda kutafuta mahali pa kuwaweka wafanyabiashara wadodo wadogo wapatao 200 wa kata hiyo waliokosa nafasi ya kufanyia biashara. Mh.Liwali amesema hayo kufuatia agizo la Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu kuagiza wafanyabiashara wote walio katika masoko yasiyo rasmi katika Manispaa hiyo kutakiwa kuondoka na kufanyia biashara zao katika masoko rasmi. Kwa mjibu wa Diwani Liwali masoko yote ambayo wafanyabiashara hao wangehamia yakiwemo soko la Mpanda Hotel lililopo kata ya Majengo na soko la Kachoma lililopo kata ya Makanyagio yote yamejaa. Wiki iliyopita,mamia ya wafanyabiashara wadogowadogo wanaofanyia biashara zao katika machinjio ya ng’ombe Mpanda Hotel waliandamana mpaka kituo cha Radio Mpanda Fm wakipinga agizo la Mkurugenzi anayewataka kuondoka katika maeneo hayo yasiyo rasmi. Kwa mjibu wa agizo la Mkurugenzi Michael Nzyungu,wafanyab

MIMBA ZA UTOTONI BADO TATIZO KULIDHIBITI

Na.Issack Gerald Tatizo la mimba za utotoni katika kata Mwamkulu Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi limekuwa gumu kulidhibiti kutokana na jamii inayoishi mahali hapo kuishi kwa kuhamahama. Hali hiyo imethibitishwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwamkulu Bw.George Iresha wakati akizungumza kuhusu namna wanavyodhibiti watoto wenye umri mdogo kupata mimba. Aidha amesema kuongezeka kwa shule za msingi na vituo shikizi vya kielimu katika kata ya mwamkulu imewapunguzia mwendo mrefu watoto ambapo umbali mrefu kutoka nyumbani mpaka shule zilipo zimekuwa zikitajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vinavyochangia mimba za utotoni. Kata ya mwamkulu yenye wakazi wapatao elfu saba ikiwa na wakazi wanaojishughulisha na kilimo na ufugaji ni miongoni mwa kata 15 za manispaa ya Mpanda. Mpaka sasa Mkoa wa Katavi unaongoza asilimia 45 kwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kati ya Mikoa yote Tanzania. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED