MIMBA ZA UTOTONI BADO TATIZO KULIDHIBITI


Na.Issack Gerald
Tatizo la mimba za utotoni katika kata Mwamkulu Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi limekuwa gumu kulidhibiti kutokana na jamii inayoishi mahali hapo kuishi kwa kuhamahama.
Hali hiyo imethibitishwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Mwamkulu Bw.George Iresha wakati akizungumza kuhusu namna wanavyodhibiti watoto wenye umri mdogo kupata mimba.
Aidha amesema kuongezeka kwa shule za msingi na vituo shikizi vya kielimu katika kata ya mwamkulu imewapunguzia mwendo mrefu watoto ambapo umbali mrefu kutoka nyumbani mpaka shule zilipo zimekuwa zikitajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vinavyochangia mimba za utotoni.
Kata ya mwamkulu yenye wakazi wapatao elfu saba ikiwa na wakazi wanaojishughulisha na kilimo na ufugaji ni miongoni mwa kata 15 za manispaa ya Mpanda.
Mpaka sasa Mkoa wa Katavi unaongoza asilimia 45 kwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi kati ya Mikoa yote Tanzania.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA