Posts

Showing posts from December 10, 2017

TAAS MKOANI KATAVI WAMEKATAA KUITWA WALEMAVU WA NGOZI

Image
Na.Issack Gerald Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania (TAAS) Mkoani Katavi kimewataka watanzania kutowaita wao kama watu wenye ulemavu wa ngozi albino badala yake wawaite watu wenye Ualbino. Mwenyekiti wa TAAS Mkoani Katavi Victus Kweka Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama hicho Mkoani Katavi Bw.Victus Kweka kupitia kikao cha kujadili kupinga ukatiri,unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za w atu wenye ulemavu kwa kuwanyima haki za msingi kama elimu,afya na haki nyingine za kibinadamu. Amesema rangi ya ngozi waliyonayo watu wenye ualbino siyo ulemavu wa ngozi bali wao wanahesabika katika kundi la watu wenye ulemavu wa macho kutokana hali waliyonayo. Kwa upande wake mratibu wa wa elimu jumuishi Wilayani Mpanda Bi.Ashura Shabaani ambaye pia ni msichana mwenye ualbino amesema mpaka sasa bado kuna baadhi ya watu wenye ualbino wanaojinyanyapaa. Amewataka watu wenye ualbino kuchanganyikana na jamii ili kupata elimu inayowawezesha kufahamu haki zao,kupatiwa mafuta ya kupu

WAZIRI WA MAJI NAYE AMTUMBUA MHANDISI WA MAJI MKOANI RUKWA

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amemsimamisha kazi Mhandisi Goyagoya Mbena kwa tuhuma za kusaini barua ya kuruhusu ujenzi wa mradi wa Maji wilayani Nkasi mkoani Rukwa. Taarifa ambayo imetolewa jana na Wizara hiyo,imeeleza kuwa Mhandisi Mbena amesaini barua kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo kinyume cha utaratibu. Mradi huo wa Maji katika kijiji cha Kamwanda Halmashauri ya Nkasi mkoani Rukwa u meelezwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 7.4. Siku ya Juzi Waziri wan chi ofisi ya Rais tawala za Mikoa na serikali za mitaa Mh.Suleiman Jafo,alimsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Julius Kawondo kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa na matumizi mabaya yaliyoisababishia Serikali hasara ya Sh 7 bilioni. Chanzo:eatv Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED