WAZIRI WA MAJI NAYE AMTUMBUA MHANDISI WA MAJI MKOANI RUKWA

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amemsimamisha kazi Mhandisi Goyagoya Mbena kwa tuhuma za kusaini barua ya kuruhusu ujenzi wa mradi wa Maji wilayani Nkasi mkoani Rukwa.
Taarifa ambayo imetolewa jana na Wizara hiyo,imeeleza kuwa Mhandisi Mbena amesaini barua kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo kinyume cha utaratibu.
Mradi huo wa Maji katika kijiji cha Kamwanda Halmashauri ya Nkasi mkoani Rukwa umeelezwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 7.4.
Siku ya Juzi Waziri wan chi ofisi ya Rais tawala za Mikoa na serikali za mitaa Mh.Suleiman Jafo,alimsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Julius Kawondo kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa na matumizi mabaya yaliyoisababishia Serikali hasara ya Sh 7 bilioni.

Chanzo:eatv
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA