Posts

Showing posts from January 20, 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMTUPA TAKUKURU MKURUGENZI MUWASA.

Image
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa ameamuru Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoani Mara kumkamata na kumuhoji Mkurugenzi Mtendani wa Mamlaka ya Maji Musoma (Muwasa) Gantala Said kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa maji Bunda. Mbali na mkurugenzi huyo pia ameiagiza Takukuru imuhoji mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Nyakirang'anyi,Mahuza Mumay ambaye ndiye mkandarasi anajenga mradi huo unaotoa maji kutoka Ziwa Victoria katika eneo la Nyabehu hadi Bunda mjini. Waziri Mkuu amefikia uamuzi huo jana baada ya mkurugenzi huyo kushindwa kueleza kitu kilichosababisha mradi wa maji Bunda kutokamilika  pamoja na Serikali kutoa fedha nyingi. Akizungumza katika kikao maalumu cha kujadili changamoto za utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Mara, alichokiitisha mjini Bunda, Waziri Mkuu alisema alimua kuitisha kikao hicho baada ya kutoridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo hususan inayosimamiwa na Muwasa. Alisema kwa sasa Serikali inatekeleza kampeni ya Rais John

SERIKALI YAKATAZA KULIMA PAMBA KWA MKATABA

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imekataza kilimo cha pamba cha mkataba kwa sababu kinawanyonya wakulima. Ameyasema hayo jana (Ijumaa, Januari 19, 2018) wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua zahanati ya Hunyari wilayani Bunda, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mara. Alisema Serikali imeweka mkakati wa kuimarisha mazao makuu ya biashara ambayo uzalishaji wake umeanza kupungua likiwemo na zao la pamba. Waziri Mkuu alisema Serikali imeamua kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa kilimo cha zao la pamba kuanzia hatua za maandalizi ya shamba,pembejeo hadi masoko. Pia Waziri Mkuu amewaagiza Maofisa Kilimo katika wilaya hiyo wawafuate wakulima vijijini kwa ajili ya kutoa elimu itakayowawezesha wakulima kulima kwa kufuata njia bora za kisasa. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wafugaji kuhakikisha wanakuwa na idadi ya mifugo kulingana na uwezo wa eneo lao.“Marufuku kulisha mifugo katika mashamba ya watu.” Amesema Serikali itachukua hatua kali za