Posts

Showing posts from January 16, 2018

WAZIRI WA MAJI ISACK KAMWELWE ATEMBELEA BWAWA LA IGOMBE TABORA ASISITIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Image
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi ISACK KAMWELWE amewataka wananchi Mkoani Tabora kutoharibu mazingira ya bwawa la Igombe ambalo kwa sasa limejaa ili kuzuia upotevu wa maji unaosababisha kero ya mgao wa maji. Waziri Kamwelwe ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Katavi Mkoani Katavi,ametoa rai hiyo alipotembelea bwawa la Igombe kukagua hali ya ujazo wa maji ambapo amesema wananchi wamekuwa wakilima pembezoni mwa bwawa hilo na kusababisha upotevu wa maji hivyo ni vyema wakaacha utamaduni huo. Amesema ili kuhakikisha wakazi wa Tabora wanaendelea kupata maji,serikali inaendelea kutekeleza mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ambapo kwa sasa tayari mabomba ya kupitishia maji tayari yameanza kufika. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Tabora-Tuwasa Mhandisi Mkama Bwire amesema ujazo wa maji katika bwawa la Igombe umeongezeka kutoka mita moja mwaka jana hadi kufikia mita 4.6 kwa sasa hali ambayo imeondoa adha ya mgao wa maji. Naye