Posts

Showing posts from June 2, 2018

ASASI ZA KIRAIA ZAINGILIA KATI SUALA LA KUONDOLEWA WALIMU WA ELIMU MAALUMU SHULENI AZIMIO

Image
Asasi za kiraia Mkoani Katavi zimelazimika kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ili kuzungumza naye kuhusu hatua ya kuwaondoa walimu waliokuwa wakifundisha watoto wenye ulemavu katika Shule ya Msingi Azimio bila kuweka wengine mbadala. Asasi hizo zimesema katika kipindi cha mwaka 2015 mpaka sasa wanafunzi wenye ulemavu hawafundishwi masomo inavyotakiwa baada ya walimu watatu kati ya watano wa elimu maalumu waliokuwepo kuondolewa katika shule hiyo na kupangiwa majukumu mengine. Zimesema,walimu watatu walioondolewa shuleni walipandishwa madaraja kuwa walimu wakuu katika shule zisizokuwa na watoto wenye ulemavu,mwingine akipandishwa daraja na kuwa mratibu elimu maalumu katika Manispaa ya Mpanda ambapo mpaka sasa amebaki mwalimu mmoja anayefundisha darasa la kwanza mpaka la saba. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu amesema hakuwa na taarifa ya kuondolewa kwa walimu hao