Posts

Showing posts from March 27, 2018

HIACE YAUA MWALIMU WA SEKONDARI KATAVI

Image
Mwalimu wa shule ya sekondari ya St.Mary’s iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Hipoliti Julius Milambo amefariki dunia papo hapo baada ya kogongwa na gari aina ya hiace. (Hiyo picha haina mahusiano na habari hii) Kwa mjibu wa mashuhuda,ajali hiyo ilitokea jana majira ya jioni ambapo marehemu aligongwa katika eneo la Mpanda Hotel na gari lililokuwa likitoka kata ya Kakese ambapo aligongwa wakati akivuka barabara. Aidha wametaja gari ambalo lilimgonga mwalimu huyo kuwa ni Hiace Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Theopister Elisha akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake amesema hajapata ripoti ya kifo cha mwalimu huyo. Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda alipotafutwa kuelezea tukio hilo amedai kuwa yupo msibani. Wakati huo huo waendeshaji wa vyombo vya moto wameshauri kuwekwa matuta katika barabara inayotoka Mpanda – Kigoma   ili kupunguza ajala za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea. Habari kamil

WANANCHI WALALAMIKIA UONEVU KATAVI

Wananchi wa kitongoji cha Itogolo katika kijiji cha Kampuni   kata ya misunkumilo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameilalamikia serikali kuwakamata,kuwatoza faini na kuwalazimisha kuvuna mazao yao kabla ya kukomaa. Wananchi hao wakiwemo Agnes John,Charles Pius na Peter Luamula wametoa malalamiko hayo katika mkutano wa hadhara wa kijiji cha Kampuni ambapo ulikuwa ukifanyika katika kitongoji hicho lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa wananachi kueleza kero zao. Wamesema wamekuwa wakikamatwa ovyo na mgambo kisha kupelekwa mahabusu na kulipishwa faini wakati hakuna elimu ya kutambua mita sitini kutoka chanzo cha maji ya mto Mpanda iliyotolewa. Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya watumia maji bonde la mto Mpanda Mahela Mahanda na Daudi Sumuni wamekanusha kuwaamrisha wananchi kuvuna mazao yao kabla ya kukomaa lakini wamekubali kuwakamata na kuwatoza faini kabla ya kutoa elimu kwa wananchi hao. Mwenyekiti wa kijiji cha Kampuni Bw.James Simoni amesema mpaka sasa watu wa

WAKURUGENZI WATATU WATUMBULIWA WAWILI WA KIGOMA

Image
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo   amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili kati ya watatu wa Halmashauri za Pangani na Kigoma baada ya kupata hati chafu katika matokeo ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2016/17. Ripoti hiyo iliyowasilishwa leo Machi 27, 2018 inaonyesha halmashauri 166   kupata hati safi,16 hati zenye shaka na halmashauri tatu kupata hati chafu. Umauzi huo unafanyika ikiwa ni dakika chache baada ya Rais John Magufuli kutoa agizo hilo. Halmashauri zilizopata hati chafu ni Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Kigoma na Pangani. Waziri Jafo amesema baada ya kuwasimamisha,amemwagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuunda timu ya watalaamu kuchunguza hati hizo na kutoa matokeo ndani ya wiki tatu. Amesema wakurugenzi waliohusika katika hati chafu ni Daud Mlahagwa (Pangani),aliyekuwa Mkurugenzi wa Kigoma Ujiji, Judethadeus Mboya ambaye amestaafu kwa sasa na