HIACE YAUA MWALIMU WA SEKONDARI KATAVI

Mwalimu wa shule ya sekondari ya St.Mary’s iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Hipoliti Julius Milambo amefariki dunia papo hapo baada ya kogongwa na gari aina ya hiace.
(Hiyo picha haina mahusiano na habari hii)
Kwa mjibu wa mashuhuda,ajali hiyo ilitokea jana majira ya jioni ambapo marehemu aligongwa katika eneo la Mpanda Hotel na gari lililokuwa likitoka kata ya Kakese ambapo aligongwa wakati akivuka barabara.
Aidha wametaja gari ambalo lilimgonga mwalimu huyo kuwa ni Hiace
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Theopister Elisha akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake amesema hajapata ripoti ya kifo cha mwalimu huyo.
Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda alipotafutwa kuelezea tukio hilo amedai kuwa yupo msibani.
Wakati huo huo waendeshaji wa vyombo vya moto wameshauri kuwekwa matuta katika barabara inayotoka Mpanda – Kigoma  ili kupunguza ajala za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea.
Habari kamili ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM   


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA