WAKURUGENZI WATATU WATUMBULIWA WAWILI WA KIGOMA


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo  amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili kati ya watatu wa Halmashauri za Pangani na Kigoma baada ya kupata hati chafu katika matokeo ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2016/17.
Ripoti hiyo iliyowasilishwa leo Machi 27, 2018 inaonyesha halmashauri 166  kupata hati safi,16 hati zenye shaka na halmashauri tatu kupata hati chafu.
Umauzi huo unafanyika ikiwa ni dakika chache baada ya Rais John Magufuli kutoa agizo hilo.
Halmashauri zilizopata hati chafu ni Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Kigoma na Pangani.
Waziri Jafo amesema baada ya kuwasimamisha,amemwagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuunda timu ya watalaamu kuchunguza hati hizo na kutoa matokeo ndani ya wiki tatu.
Amesema wakurugenzi waliohusika katika hati chafu ni Daud Mlahagwa (Pangani),aliyekuwa Mkurugenzi wa Kigoma Ujiji, Judethadeus Mboya ambaye amestaafu kwa sasa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Kigoma Hanji Godigodi na Damian Chambasi wa Pangani.
Amesema taarifa itakayopatikana itabainisha kiwango cha uchafu huo na Serikali itachukua hatua nyingine za kisheria kadri uchunguzi utakavyoelekeza.
Aidha amewataka wakurugenzi katika halmashauri zilizofanya vizuri katika ukaguzi huo,waendelee kutekeleza na majukumu yao na kutoa majibu ya hoja zote zilizobainishwa na ripoti ya CAG.
Amesema Serikali imeanza kufanya vizuri katika ukaguzi huo baada ya kufikia asilimia 90 na matumaini yaliyopo ni kuondokana na taarifa ya hati chafu ili kuhakikisha fedha za Serikali zinatumika kwa maendeleo ya wananchi.
Habari kamili ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM    

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA