Posts

Showing posts from November 14, 2017

CHANGAMOTO SKIMU YA UMWAGILIAJI RUKWA, MKUU WA MKOA ATOA AGIZO KALI KWA WAFUGAJI WA MIFUGO

Image
Na.Issack Gerald MRADI wa skimu ya umwagiliaji ya Ng'ongo wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa,unazidi kupungua uwezo wa kuzalisha mazao siku hadi siku kutokana na ukosefu wa maji pamoja na wafugaji wanaofuchungia mifugo katika eneo hilo. Akizungungumza jana mbele ya mkuu wa mkoa wa Rukwa,mwenyekiti wa mradi wa scheme ya umwagiliaji ya Ng'ongo Justine Amon alisema kwa kipindi cha mwaka 2015 /2016 wakulima walilima hekta 128 na kufanikiwa kuzalisha tani 460.8 za mahindi. Alisema katika msimu wa mwaka 2016/2017 katika hekta hizo 128 uzalidhaji umeshuka hadi kufikia tani 358.4 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo haribifu wa mazingira pamoja na wafugaji kuchungia ndani ya eneo la uzalishaji.   Amon alisema eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hekta 630 lakini zinazolimwa ni hizo 128 tu kwa kuwa ujenzi wa mfereji wenye urefu wa mita 3,000 haujakamilika kwa muda mrefu sasa. Mpaka sasa mfereji uliokalimilika unaurefu wa mita 1,725 ambao ndiyo unatumika katika umwagiliaji wa h

WANANCHI WILAYANI SUMBAWANGA MKOANI RUKWA KULIPWA FIDIA KABLA YA UPANUZI UWANJA WA NDEGE

Image
Na.Issack Gerald WIZARA ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano imewahakikishia kuwalipa fidia wananchi wanaozunguka uwanja wa ndege Sumbawanga Mkoani Rukwa kabla ya kuanza upanuzi na ujenzi. Uwanja wa ndege wa Sumbawanga kabla ya kuharibika Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa wizara hiyo Mh .Elias John Kwandikwa wakati akijibu swali la mbunge viti maalumu mkoani Rukwa Bupe Mwakang’ata aliyetaka kujua lini upanuzi na ujenzi wa uwanja wa ndege Sumbawanga utakamilika pamoja na kuwalipa fidia wananchi hao. Amesema wananchi wa Sumbawanga waendelee kuvumilia kwani muda wowote watalipwa fidia na kuongeza kuwa sheria itazingatiwa ikiwa wananchi hawatalipwa fidia zao kwa wakati ili walipwe fidia ya ziada. Aidha waziri Kwandikwa amesema mwezi Oktoba Mwaka 2016 serikali ilisaini mkataba na Kampuni ya SMPC kutoka Australia ili kusimamia ujenzi wa uwanja huo. Wakati huohuo mwezi Juni mwaka huu,serikali ilitiliana saini mkataba na kampuni ya Sino Shine Over Seas Construction And In

JAMII MKOANI KATAVI IMETAKIWA KUSHIRIKI KUWAFICHUA WATOTO WENYE ULEMAVU WALIOFICHWA MAJUMBANI ILI WAPATE HAKI YAO YA ELIMU

Image
Na.Issack Gerald-Katavi JAMII Mkoani Katavi imeaswa kushirikiana ipasavyo na kamati ya kulea baraza la watoto wenye ulemavu iliyopo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi kwa kuwafichua watoto waliofichwa majumbani ili wapatiwe haki ya elimu. Wanafunzi wenye ulemavu na wasio na ulemavui katika shule ya msingi Azimio Manispaa ya Mpanda wakiwa katika picha ya pamoja(PICHA NA.Issack Gerald) Aliyevaa koti kutoka kushoto ni mratibu wa Mradi wa elimu Jumuishi Mkoani Katavi,wa pili Issack Gerald mwandishi Mpanda Radio fm pia mjumbe na katibu wa kamati hiyo,waliobaki ni baadhi ya watoto wenye ulemavu (PICHA NA.Issack Gerald) Wito huo umetolewa leo na Meneja wa Mradi wa elimu jumuishi Tanzania Alani Kamunde wa shirika la International Aid Services,kupitia kikao cha kupokea,kujadili,kutathimini na kupanga mikakati ya namna ya kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayowakbili watoto wenye ulemavu Mkoani Katavi. Kwa upande wake mratibu wa mradi wa elimu Jumuishi mikoa ya Rukwa na Katavi Bi.Veronic