CHANGAMOTO SKIMU YA UMWAGILIAJI RUKWA, MKUU WA MKOA ATOA AGIZO KALI KWA WAFUGAJI WA MIFUGO
Na.Issack Gerald

Akizungungumza jana mbele ya mkuu wa mkoa wa Rukwa,mwenyekiti wa mradi wa scheme ya umwagiliaji ya Ng'ongo Justine Amon alisema kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 wakulima walilima hekta 128 na kufanikiwa kuzalisha tani 460.8 za mahindi.

Amon alisema eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni hekta 630 lakini zinazolimwa ni hizo 128 tu kwa kuwa ujenzi wa mfereji wenye urefu wa mita 3,000 haujakamilika kwa muda mrefu sasa.
Mpaka sasa mfereji uliokalimilika unaurefu wa mita 1,725 ambao ndiyo unatumika katika umwagiliaji wa hekta hizo 128 ambazo wakulima wanafanya kilimo cha umwagiliaji mara mbili kwa mwaka ukitegemewa na vijiji vya Ng'ongo,Mwela na Mtowisa wakijishghulisha na kilimo cha mahindi,mpunga,nyanya na vitunguu.
Kwa mjibu wa mwenyekiti huyo,wakulima wangenufaika zaidi iwapo mradi huo ungekamilika kwani wapo baadhi ya wananchi wanatamani kulima wanashindwa kutokana na kutokamilika kwa mradi huo.
Wahisani walitoa shilingi milioni 600 ili kujenga mradi huo uwanufaishe wananchi lakini walio wengi wameshindwa kunufaika kutokana na mradi huo kutokamilika kwa muda mrefu hivyo wanaiomba halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga itafute fedha ili kukamilisha mradi huo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amesema ili uzalishaji uongezeka ni lazima sheria ndogo za halmashauri zitumike kuwabana waharibifu wa mazingira.
Amesema bonde la ziwa Rukwa limeelemewa na mifugo maratatu zaidi ya uwezo wake na hivyo amewataka wafugaji wapunguze mifugo ambapo kwa atakayeshindwa kukubaliana na agizo lake basi aondoke mkoani Rukwa akatafute sehemu watakayo mpokea.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments