Posts

Showing posts from June, 2016

MKOA WA KATAVI WAREJESHA MIL.56 ZA WATUMISHI HEWA

Mkoa wa Katavi umefanikiwa Kurejesha fedha za watumishi hewa kwa asilimia 23.34 ambapo ni   kiasi cha zaidi ya shilingi   milioni 56   kati ya   milioni   zaidi ya 240 zimelipwa kama mishahara hewa.

HUYU NAYE WIKI HII KADAKWA NA MENO MAWILI YA TEMBO WILAYANI MLELE,MWINGINE NAYE AIBA MPUNGA SHAMBANI AKAMATWA NA WANANCHI ACHOMWA MOTO HADI KIFO.

JUNI 14 mwaka huu,Jeshi la Polisi lilimkamata Oscar Pius Mizengo (30) mkazi wa Kitongoji cha Inyagala - Ikuba Kijiji cha Nyakasi kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi akiwa na meno mawili ya tembo yenye uzito wa kilogramu 32 moja likiwa na urefu wa sentimita 150 na lingine 148 cm ambayo thamani yake ni Tsh 30,000,000/= milioni thelasini sawa na tembo mmoja aliyeuwawa.

WIKI HII MAMA WA WATU JERA MIEZI SITA KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA GONGO

Mahakama ya wilaya mjini Mpanda imemhukumu mtu mmoja kifungo cha miezi sita jera au kulipa faini kiasi cha shilingi laki moja   kwa kosa la kukutwa na pombe haramu.

KUHUSU UCHANGIAJI DAMU SALAMA WIKI HII MKOANI KATAVI,SERIKALI YA MKOA YATUPIWA LAWAMA KUTOUNGA MKOANO ZOEZI HILO

Juni 14 wiki hii ilikuwa ni kilele cha Siku ya uchangiaji damu salama kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji huduma ya kuongezewa damu. Miongoni mwa wahitaji wakubwa wa damu ni pamoja na mama wajawazito ,watoto wenye umri chini ya miaka    5 pamoja na wagonjwa mbali mbali wenye uhitaji wa huduma hiyo.

JERA MIEZI 6 MPANDA AKITUHUMIWA KUJIPATIA FEDHA KWA UDANGANYIFU

Mahakama ya mwanzo mjini mpanda imemhukumu mtu mmoja kwenda jera     miezi sita au kulipa faini ya shilingi laki mbili kwa kosa la kujipatia   fedha kwa   njia ya udanganyifu.

KATAVI YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO AFRIKA,NDANI YA MIEZI 6 WATOTO ZAIDI YA 30 WAFANYIWA UKATIRI KATAVI

Mkoa wa Katavi umeadhimisha maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika    ambapo maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili.

WATANZANIA WAPYA KATUMBA WATAKIWA KUTOKARIBISHA WAGENI KINYUME CHA SHERIA

WATANZANIA waliopewa Uraia katika Makazi ya Katumba Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mlele, Mkoani Katavi, wametakiwa kuacha kuwakaribisha watu wanaoingia nchini kinyume cha sheria.

4 HAMAHAKAMANI KWA KUINGIA MGODINI BILA IDHINI YA MMILIKI

WATU wanne wamefkishwa katika mahakama ya mwanzo mjini mpanda kwa kosa la kuingia mgodini bila idhini ya mmiliki wa mgodi huo.

YALIYOMKUTA ALIYEKAMATWA NA JINO MOJA LA TEMBO MKOANI KATAVI LENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.1 HAYA HAPA

MTU mmoja mkazi wa Mgorokani Matandarani wilaya ya   Mlele mkoni Katavi amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mpanda   kwa makosa mawili tofauti likiwemo la kukutwa na jino 1 la tembo lenye thamani ya shilingi milioni thelasini.

BARABARA YA MPANDA TABORA KUPITIA MTO KOGA YAFUNGULIWA

BARABARA inayoanzia Mpanda hadi Tabora kupitia daraja la mto Koga imefunguliwa na magari kuruhusiwa kutumia barabara hiyo kwa safari.

AHUKUMIWA JERA MIEZI 6 AU FAINI KWA SHAMBULIO LA KUTUMIA MWIKO

MAHAKAMA ya mwanzo mjini Mpanda imemuhukumu mtu mmoja mkazi wa Shanwe   kifungo   cha miezi 6 jera au kulipa faini   ya   shilingi laki mbili.

WAKAZI KATA YA KAZIMA WALALAMIKIA MANISPAA YA MPANDA KUTOPIMIWA VIWANJA VYAO KWA MIAKA 9 SASA

Wakazi wa kata ya kazima manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameulalamikia uongozi wa   halimashauri hiyo kushindwa kuwapimia viwanja takriban miaka tisa, hali iliyowalazimu baadhi yao kuanza ujenzi wa maeneo hayo bila kupimwa.

LATCU KATAVI WASHAURIWA KUWEKEZA UJENZI WA MAJENGO KUJIIMARISHA KIUCHUMI

MKUU wa mkoa wa Katavi meja generali mstaafu   Raphaeli Muhuga amesema chama kikuu cha ushirika cha   wakulima wa tumbaku LATCU   kinaweza kupata ufanisi zaidi kama kitaendeleza jitihada zake za kuwekeza katika ujenzi wa majengo kama vitega uchumi.

TFDA KATAVI YATEKETEZA TANI 2 ZA BIDHAA BANDIA ZENYE THAMANI ZAIDI YA SHILINGI MIL.6

Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini FFDA Kanda ya Magharibi Imeteketeza bidhaa mbalimbali   zisizofaa katika matumizi ya binadamu   zenye thamani ya shilingi Milioni 6 na laki 5 Ambazo ni sawa na tani 2 zilizoingizwa Kinyemela nchini.

MATUKIO YA MAJANGA YA MOTO YAENDELEA KUTIKISA KATAVI

Jumla ya watu watatu kati ya saba waliopatwa na majanga ya moto wamefariki dunia katika matukio sita yaliyotokea yakihusisha majengo na vyombo vya usafiri.

WAISLAMU KATAVI WAJIAANDA MFUNGO WA RAMADHANI,WANAKATAVI WAPEWA NENO

Leo ni siku ya mwisho ya siku ya Shaabani katika dini ya kiislamu ikimaninisha siku ya mwisho kabla ya mfungo wa siku ya ramadhani kuanza hapo kesho.

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE MIEZI 6 KWA UBADHIRIFU WA FEDHA

Mahakama ya mwanzo mjini Mpanda imemhukumu mtu mmoja kifungo cha nje miezi sita kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka kwa kutumia fedha bila kufuata utaratibu wa ofisi.

TRL KATAVI KUBORESHA MIUNDOMBINU USAFIRI WA TRENI

SHIRIKA la reli mkoni katavi limeanza kuboresha miundombinu ya   Reli pamoja na mabehewa ili kutoa huduma bora ya Usafiri kwa watumiaji.