Posts

Showing posts from March 18, 2018

TRA YATUMBUA WAFANYAKAZI WAWILI

Image
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewasimamisha kazi watumishi wake wawili mkoani Lindi,kwa kile kilichodaiwa kwenda kinyume na kanuni na miongozo ya kazi inavyowaelekeza na kutumia lugha isiyo rafiki na wateja wao {wafanyabiashara}. Uamuzi huo,umechukuliwa na Kamishina kodi ya Mapato za ndani nchini,Elijah Mwandumbya,wakati wa kikao cha pamoja kati yake na wafanyabiashara wa mkoa huo kilichofanyika Manispaa ya Lindi baada ya kusikiliza malalamiko mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara hao. Mwandumbya amesema Taifa wamekuwa wakipata taarifa kwamba hakuna mahusiano mazuri kati watumishi hao na wafanyabiashara,hali iliyohustua uongozi na kumtuma Kamishina huyo kufika mkoani humo kupata maelezo ya kina. Kamishina huyo wa kodi za ndani amesema {TRA} inapitia kipindi ambacho kinahitaji kuwapatia huduma bora wateja wao ili waweze kumsaidia Rais wa nchi katika utekelezaji wake wa maendeleo kwa kuhakikisha wanazingatia Sheria,kanuni,taratibu na miongozo,kuhakikisha wanatoa huduma ili

MH.MKAPA AIBUKIA SEKTA YA ELIMU ATAKA MJADALA KITAIFA

Image
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamini William Mkapa ametaka kuitishwa mjadala wa kitaifa wa kujadili hali ya elimu nchini kufuatia shule za serikali kuendelea kufanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kitaifa. Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Benjamini William  Mkapa ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma amesema hayo mkoani Dodoma wakati wa tukio la kumuingiza kazini Makamu Mkuu mpya wa chuo kikuu hicho cha Dodoma Profesa Egid Mubofu. Katika tukio hilo wamemuaga Makamu Mkuu wa chuo hicho aliyemaliza muda wake Profesa Idrisa Kikula. Mhe.Mkapa amesema mjadala huo unatakiwa kuhusisha makundi yote ya jamii bila kujali kama ni ya sekta binafsi au ya umma sambamba na watu wa kawaida siyo wasomi pekee ambapo kupitia njia hiyo anaamini suluhu ya kudumu itapatikana. Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM