Posts

Showing posts from January 10, 2018

RC RUKWA APIGA MARUFUKU KUPAKIA MIZIGO KATIKA MWALO WA KIRANDO

Image
SERIKALI mkuu mkoani   Rukwa imepiga marufuku   kuutumia mwalo uliopo katika   Kijiji cha Kirando ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupakia na kushia mizigo kwani mwalo huo umetengwa kwa ajili ya shughuli za kuuzia samaki. Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alisema hayo akiwa katika ziara ya kikai wilayani Nkasi na kukuta katika mwalo wa Kirando unatumika kama bandari ambapo malori yalikuwa yakipakua na kupakia mizigo kwa lengo la kusafisirisha  kuipeleka kwenye visiwa vilivyopo ziwa Tanganyika. Alisema kuwa wananchi wasipotoshe lengo la kutebnwa kwa  mwalo huo ambayo ni kwaajili ya kuuza na kununua samaki wavuliwao kwenye ziwa Tanganyika na si  kwaajili ya magari kupakilia mizigo. Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa sehemu iliyotengwa ikitumika kama bandari haiko vizuri basi waone namna ya kuboresha ili sehemu hiyo ilirudi kama ilivyokuwa na sio kuikimbia na kuiacha kama ilivyo jwani kukimbia tatizo sio suluhisho bali kupambana na changamoto zilizopo na kuboresha. Awali kabla ya Kukarib

DC MKOANI RUKWA APIGA MARUFUKU WAGONJWA WA KIPINDU PINDU KUPELEKWA KWA WAGANGA WA JADI

Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa Dk.Halfan Haule amewataka wakazi wa bonde ziwa Rukwa,kuacha tabia ya kuwapeleka wagonjwa wa kipindupindu kwa waganga wa kienyeji badala yake wawapeleke vituo vinavyotoa huduma za afya ili kupata tiba za kitaalamu. Mkuu huyo wa wilaya alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mtowisa wilayani Sumbawanga mkoani humo. Alisema tabia ya baadhi ya wananchi kuendekeza imani za kushirikina na kuwapeleka wagonjwa wa kipindupindu kwa waganga wa kienyeji kunahatarisha maisha ya wagonjwa hao na wakati mwingine kusababisha vifo. Alisema jamii ya watu wa bonde la ziwa Rukwa ambako ugonjwa huo umeenea ipo haja sasa kubadilika na kuachana na tabia hiyo kwani ugonjwa huo unatokana na uchafu na si  kulogwa hivyo wanapaswa  kuwapeleka wagonjwa  katika zahanati,vituo vya afya na hospitali ili wapate tiba sahihi ambazo zitaokoa maisha yao. Aidha Dk.Haule alipiga marufuku tabia ya kaya moja kutumia choo kimoja badala yake alitaka kila kaya kuw

WAFANYABIASHARA WILAYANI MPANDA WASITISHA MGOMO WA SIKU MBILI

Image
Mamia ya wafanyabiasahara katika masoko ya Mpanda Mkoani Katavi leo wameanza kufanya biashara kama kawaida kufuatia kuwepo kwa mgomo huo kwa muda wa siku mbili. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema wamefanya mazungumzo na uongonzi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Katavi ili kufikia mwafaka wa mgomo uliosababishwa na kupandishwa kwa bei ya Pango kutoka sh 15,000 kwa hapo awali na kufikia shilingi 60,000. Kwa upande wa Mwenyekiti wa Soko la Buzogwe ambalo ni kitovu cha mvutano huo Bw.Ramadhani Karata  amedai amekuwa  mafichoni  kwa muda kutokana na kuandamwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za yeye kuwa chanzo. Mgomo wa wafanyabiashara hasa katika soko kuu la Wilaya ya Mpanda na Soko la Buzogwe ulianza juzi ambapo Mkuu wa Wilaya alikuwa amesisitiza kuwa mfanyabiashara asiyetaka kulipa tozo hizo arudishe chumba cha biashara. Hata hivyo mwafaka kamili kuhusu kiasi ambacho kinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara kinatarajiwa kutolewa baada ya wiki moja hiyo ikiwa ni kwa mjibu wa