Posts

Showing posts from March 25, 2018

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

Image
Jokate Mwegelo Jokate Mwegelo Amezaliwa Jokate Urban Mwegelo 20 Machi   1987   (umri 31) 20 Machi   1987   (umri 31) Utaifa MTanzania Mhitimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ( Shahada ya Sayansi ya Siasa ) Kazi yake Mwigizaji, mjasiriamali, mtangazaji, mwimbaji Miaka ya kazi 2006-hadi sasa Jokate Mwegelo  ni  mwigizaji  wa  filamu  na mjasiriamali kutoka nchini  Tanzania . Jokate vilevile ni mtangazaji na mwimbaji. Huyu ni  Afisa Mtendaji Mkuu  wa kampuni ya  Kidoti Company .Mwaka wa 2011,alishinda tuzo ya  Zanzibar International Film Festival  akiwa kama mwigizaji bora filamu wa kike.Mwaka wa 2017,Mwegelo aliingizwa katika jarida la Forbes katika  Forbes 30 Under 30  kutoka Afrika. MAISHA YA AWALI NA ELIMU. Mwegelo alizaliwa mnamo tarehe 20 Machi,1987 huko mjini  Washington D.C ambapo wakati huo wazazi wake walikuwa wanafanya kazi.Alikulia jijini  Dar es Salaam, Tanzania .Alianza elimu y

JOKATE ATUMBULIWA UVCCM

Image
Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM iliyokutana kwa dharura mchana huu chini ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Kheir Denis Jemes imetengua uteuzi wa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa Jokate  U. Mwengelo kuanzia leo. Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia mtandao wa twitter wa UVCCM imesema kuwa Jokate Mwegelo ametenguliwa katika nafasi hiyo ambapo amehudumu katika nafasi hiyo kwa takribani miezi 11 toka amelipoteuliwa April 2017.  Kikao hicho kilichomtengua Jokate kiliendeshwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Ndg.  Kheri Denis James (MCC) katika ukumbi wa secretariet  White house Mjini Dodoma lakini bado hawajaweka wazi sababu zilizopelekea kutengua uteuzi wa Jokate Mwegelo.  Jokate Mwegelo Amezaliwa Jokate Urban Mwegelo 20 Machi   1987   (umri 31) Utaifa MTanzania Mhitimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ( Shahada ya Sayansi ya Siasa ) Kazi yake

RAIS MAGUFULI KUPOKEA MAGARI 181 YA KUSAMBAZIA DAWA NCHINI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kupokea magari 181 yatakayokuwa yakitumika kusambaza madawa vijijini na mjini. Kwa mjibu wa taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt. Hassan Abbas Rais Magufuli ndiye atakuwa mgeni rasmi na kuzindua magari hayo 181. Magari hayo yapo chini ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na yataongeza ufanisi katika kufikisha huduma katika maeneo yaliyokuwa hayafikiwi. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

UYOGA WAUA WAWILI KATAVI NA WENGINE MAHUTUTI

Image
Watu wawili ambao wametambulika kwa majina Frenki Mayaga na Erizabeth George wakazi wa kijiji cha   Stalike wilayani Mpanda mkoani Katavi,wafamefariki dunia baada ya kula uyoga unaotajwa kuwa na Sumu. Mwenyekiti wa Kijiji hicho Christopher   Anjero amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo leo ambapo amesema mbali na marehemu hao,watu wengine watatu wako mahututi na wanaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mpanda. Bi.Monica George ambaye ni miongoni mwa ndugu wa marehemu amesema walikwenda porini kutafuta uyoga ambapo baada ya kupika na kula ndiyo wakapatwa na mauti hayo. Aidha George Anjero Mrisho amesema alipokea taarifa za kifo cha kijana wake Frenki Mayaga akiwa shambani. Hata hivyo Mganga wa zamu wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda hakuupatikana ili kujua taratibu za kitabibu zinazoendelea kwa sababu hakuwepo kituoni. Kwa mjibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike Bw. Christopher   Anjero hilo ni tukio la kwanza katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ndani ya uon

MAASKOFU WAANZA KUTEMA CHECHE SUALA LA KATIBA MPYA NA USALAMA WA TAIFA

Image
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dk.Fredrick Shoo amesema kama taifa linahitaji maendeleo ya kweli basi kuna haja ya kuwa na katiba mpya na si iliyopo sasa.  Askofu Dk.Fredrick Shoo  Askofu Dk Fredrick Shoo alisema hayo baada ya kutoa ujumbe wa Pasaka na kusema kuna haja ya kuwa na katiba mpya ili kuweza kupata maendeleo ya kweli kwani katiba mpya ndiyo inaweza kuongoza kila raia.  "Katiba iongoze kila raia, utaratibu wa Watanzania kuweza kuishi pamoja na kama tunataka maendeleo ya kweli pasipo Katiba mpya tutakuwa tunajidanganya"  alisema Askofu Shoo  Mbali na hilo Askofu Shoo aliweza kuzungumzia mambo mengi kuhusu usalama wa nchi na watu wake na kuonyesha wasiwasi kuwa kuna vitu haviendi sawa kutokana na kuibuka kwa mambo ambayo si utamaduni wa Tanzania, kama watu kupigwa risasi, kuokotwa kwa miili ya watu baharini, kuuwawa kwa watu katika mazingira ya kutatanisha. Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM