Posts

Showing posts from November 25, 2017

RAIS MAGUFULI ASISITIZA JENGO LA TANESCO KUBOMOLEWA

Na.Issack Gerald Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amesisitiza kuwa jengo la TANESCO Ubungo ni lazima libomolewe kwa sababu yeye ndiye rais kwa sasa tofauti na zamani alipokuwa waziri. Rais amesema hayo mapema leo wakati akihutubia wananchi ambao wamejitokeza katika ufunguzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila. Aidha rais Magufuli amesema Jengo hilo lazima libomolewe hata nusu ya jengo iliyopoo katika hifadhi ya barabara huku akisema na kama ni kuondoa jengo lote basi inamaanisha kuwa pia jengo la wizara ya maji nalo itabidhi liondolewe kwa kuwa sheria ni msumeno. Wakati huo huo rais amesema wakazi wa Kimara ambao nyumba zao zimebomolewa hawatalipwa fidia kwa sababu zilikuwa ndani ya hifadhi ya barabara na waliotakiwa kulipiwa fidia walikwishalipwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MKOA WA KATAVI UMEZINDUA SIKU 16 ZA KUPAMBA NA AKATIRI WA KIJINSIA

Na.Issack Gerald Mkoa wa Katavi umezindua siku 16 za kupinga ukatiri wa Kijnsia uzinduzi ambao umefanyika katika kata ya Kabungu wilayani Tanganyika ambapo kilele chake kitakuwa Desemba 12 mwaka huu. Akizungumza katika uzinduzi huo,kamanda wa Polisi mkoani Katavi Damasi Nyanda amesema makosa ya ubakaji yamepungua kutoka matukio 100 kwa mwaka na kufikia matukio 68 kwa mwaka huu ambayo yameripotiwa. Aidha Kamanda Nyanda amewapongeza wananchi kwa kuendelea kushirikiana na jeshi hilo katika kutoa taarifa mbalimbali ikiwepo za ukatili unaoendelea kutokea sehemu mbalimbali za mkoa huu. Kwa upande wao wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Katavi katika risala yao wameomba mkoa kutafuta njia za kupunguza au kumaliza tatizo la mimba za utotoni kwa kuwa ni miongoni mwa sababu inayosababisha vifo kwa watoto wengi kutokana na uzazi. Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa katavi Meja jenerali Rafaeli Muhuga mgeni rasmi katika uzinduzi huo amewataka wananchi kuacha kufuata mila potofu zi

RAIS MAGUFULI KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA UHURU KENYATTA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli anatarajiwa kuungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mteule Mh.Uhuru Kenyatta. Taarifa ya serikali ambayo imetolewa na Mkurugenzi, Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi imethibitisha hilo. Mhe.Kenyatta anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumanne ya wiki ijayo jijini Nairobi ikiwa ni baada ya kushinda uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini humo. Rais Uhuru Kenyatta atakuwa anaongoza Jamhuri ya Kenya kwa kipindi cha awamu ya pili. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

WANANCHI MKOANI KATAVI WATAKIWA KUTOIOGOPA MAHAKAMA

Na.Issack Gerald Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa kutoiogopa mahakama kwa kuwa ipo kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wananchi katika kupatikana na kwa haki zao. Wito huo umetolewa na hakimu mwandamizi wa mahakama ya mwanzo mjini Mpanda Mh.David Daniel Mbembela kupitia kipindi cha kumekucha Tanzania kinachorushwa cha Mpanda Radio. Aidha amewashauri wananchi kujenga tabia ya kufika katika mahakama kwa ajili ya kujifunza namna kesi zinavyoendeshwa mahakamani. Wakati huo huo Mh.Mbembela amesema serikali imeleta baraza la ardhi la wilaya mkoani Katavi kwa ajili ya kusikiliza migogoro na kesi zinazohusu masuala ya ardhi ambapo awali wakazi wa Mkoa wa Katavi walikuwa wakipata huduma hiyo wilayani Sumbawanga Rukwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS MAGUFULI AMEMTEUA DKT SLAA KUWA BALOZI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe amemteua Dkt.Wilbrod Peter Slaa kuwa Balozi. Kwa mjibu wa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ya Rais,Dkt.Wilbrod Peter Slaa ataapishwa baada ya taratibu kukamilika. Habari zaidi ni P5TANZANI ALIMITED