MKOA WA KATAVI UMEZINDUA SIKU 16 ZA KUPAMBA NA AKATIRI WA KIJINSIA

Na.Issack Gerald
Mkoa wa Katavi umezindua siku 16 za kupinga ukatiri wa Kijnsia uzinduzi ambao umefanyika katika kata ya Kabungu wilayani Tanganyika ambapo kilele chake kitakuwa Desemba 12 mwaka huu.
Akizungumza katika uzinduzi huo,kamanda wa Polisi mkoani Katavi Damasi Nyanda amesema makosa ya ubakaji yamepungua kutoka matukio 100 kwa mwaka na kufikia matukio 68 kwa mwaka huu ambayo yameripotiwa.
Aidha Kamanda Nyanda amewapongeza wananchi kwa kuendelea kushirikiana na jeshi hilo katika kutoa taarifa mbalimbali ikiwepo za ukatili unaoendelea kutokea sehemu mbalimbali za mkoa huu.
Kwa upande wao wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Katavi katika risala yao wameomba mkoa kutafuta njia za kupunguza au kumaliza tatizo la mimba za utotoni kwa kuwa ni miongoni mwa sababu inayosababisha vifo kwa watoto wengi kutokana na uzazi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa katavi Meja jenerali Rafaeli Muhuga mgeni rasmi katika uzinduzi huo amewataka wananchi kuacha kufuata mila potofu zinazopelekea matukio kikatili.
Uzinduzi huu ufanyika samabamba na mkoas wa katavi Kuanzimisha miaka 5 tangu ulipopewa hadhi ya kuwa Mkoa Novemba 25,2012.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA