Posts

Showing posts from April 9, 2018

RC RUKWA AFANIKISHA ENEO LA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amefanikisha kupatikana kwa ekari 3 ili kujengwa kwa nyumba za askari polisi katika eneo la karibu na kituo cha polisi kipya kinachomaliziwa kujengwa katika kata ya Mtowisa,Wilayani Sumbawanga na kurahisisha makazi ya polisi katika bonde la ziwa Rukwa. Hayo yamejiri ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya wananchi wa kata ya Mtowisa kwa Mkuu wa Mkoa waliyoiahidi tarehe 13.11.2017 Mh.Wanagabo alipofanya ziara katika eneo hilo na kudai kuwa usalama wa bonde hilo sio mzuri kwa kukosa kituo bora cha polisi na makazi yao na kupelekea kuanzisha ujenzi wa kituo na hatimae kuomba nguvu ya Mkuu wa Mkoa kuweza kumalizia ujenzi huo. Mtendaji wa Kata ya Mtowisa Paulo Katepa alimuhakikishia MKuu wa Mkoa kuwa eneo hilo limeshapatikana na tayari kwa kukabidhi kwa askari polisi kwaajili ya taratibu nyingine za kisheria na kumuhakikishia kuwa eneo hilo halihitaji fidia ya aina yoyote na kwamba wananchi wa Kijiji cha Mtowisa wameridhia bila ya kusukumwa, na

WAKAZI WALALAMIKA KITUO CHA AFYA KUKOSA CHUMBA CHA KUHIFAHIDHIA MAITI

Image
WAKAZI wa kata ya mtowisa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wamelalamikia kitendo cha kituo cha afya Mtowisa ambacho ni kikongwe kwa zaidi ya miaka 20 kutokuwa na chumba cha kuhifadhia maiti kitendo kinachosababisha wagonjwa kukaa na maiti muda mrefu wodini baada ya mtu kufariki. Wakizungumza mbele ya mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi na kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho.  Wakazi hao walimweleza mkuu huyo wa mkoa kuwa wagonjwa wanalazimika  kulala na miili ya marehumu wardini  huku wakisubiri ndugu wa marehamu kufika na kuchukua miiili hiyo kwa maziko na wakati mwingine maziko ya baadhi ya watu yamekuwa yakifanyika haraka bila kusubiri ndugu wa karibu na marehemu hao kutokana na kuzikwa mapema kwa kuhofia kuharibika kutokana na  kukosekana chumba cha kuhifadhia maiti. Mmoja wa wakazi hao  Christina Mponji alisema kuwa iwapo kifo kikimfika mgonjwa aliyekuwa amelazwa jirani na kitanda chako hali inayosababisha kupatwa na hofu jamb

MAHAKAMA KUTOA HUKUMU KESHO MKOANI KATAVI

Image
Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Mh.Chigangwa Tengwa amesema kesho Aprili 10,2018 inatarajia kutolewa hukumu dhidi ya Kigalu Huba mkazi wa kijiji cha Kambuzi Halt wilayani Mpanda Mkoani Katavi anayekabiliwa na kosa la kukutwa na risasi 12 za silaha aina ya kivita   ya AK47. Mh.Tengwa amefikia uamuzi huo leo baada ya kusikiliza mashahidi wa pande zote mshtaki na mshtakiwa. Awali mkuu wa mpelelezi mkoani Katavi Emmanuel Parangyo ameiambia mahakama hiyo kuwa Bw.Humba alipatikana na hatia hiyo Tarehe 19 Machi,2018   katika nyumba anayoishi. Aidha Parangyo ameiambia mahakama kuwa mwananchi haruhusiwi kumiliki risasi au silaha ya kivita kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi ya Tanzania. Mmoja wa mashuhuda upande wa washtaki akiwemo Mwenyekiti wa kijiji cha Kambuzi Halt Bw.Tuamin Elly,Bw.Huba alikuwa akilalamikikiwa na wananchi kwa kujihusisha na matukio ya uhalifu mara kwa mara. Hata hivyo mtuhumiwa amekana mashtaka dhidi y