RC RUKWA AFANIKISHA ENEO LA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amefanikisha kupatikana kwa ekari 3 ili kujengwa kwa nyumba za askari polisi katika eneo la karibu na
kituo cha polisi kipya kinachomaliziwa kujengwa katika kata ya Mtowisa,Wilayani Sumbawanga na kurahisisha makazi ya polisi katika bonde la ziwa Rukwa.
Hayo yamejiri ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya wananchi wa kata ya Mtowisa kwa Mkuu wa Mkoa waliyoiahidi tarehe 13.11.2017 Mh.Wanagabo alipofanya ziara katika eneo hilo na kudai kuwa usalama wa bonde hilo sio mzuri
kwa kukosa kituo bora cha polisi na makazi yao na kupelekea kuanzisha ujenzi wa kituo na hatimae kuomba nguvu ya Mkuu wa Mkoa kuweza kumalizia ujenzi huo.
Mtendaji wa Kata ya Mtowisa Paulo Katepa alimuhakikishia MKuu wa Mkoa kuwa eneo hilo limeshapatikana na tayari kwa kukabidhi kwa askari
polisi kwaajili ya taratibu nyingine za kisheria na kumuhakikishia kuwa eneo hilo halihitaji fidia ya aina yoyote na kwamba wananchi wa Kijiji cha Mtowisa
wameridhia bila ya kusukumwa, na kufanya yote kwaajili ya usalama wao na wa mali zao.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoawa Rukwa ACP George Kyando amekiri kupokea eneo hilo la ekari 3 na kuahidi kuwatuma vijana wake ili waanze maandalizi ya kuweka alama zinatakazobainisha eneo hilo na maeneo
mengine ili waendelee na taratibu nyingine za kisheria ili kumiliki eneo hilo kihalali.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA