MAHAKAMA KUTOA HUKUMU KESHO MKOANI KATAVI


Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Mh.Chigangwa Tengwa amesema kesho Aprili 10,2018 inatarajia kutolewa hukumu dhidi ya Kigalu Huba mkazi wa kijiji cha Kambuzi Halt wilayani Mpanda Mkoani Katavi anayekabiliwa na kosa la kukutwa na risasi 12 za silaha aina ya kivita  ya AK47.
Mh.Tengwa amefikia uamuzi huo leo baada ya kusikiliza mashahidi wa pande zote mshtaki na mshtakiwa.
Awali mkuu wa mpelelezi mkoani Katavi Emmanuel Parangyo ameiambia mahakama hiyo kuwa Bw.Humba alipatikana na hatia hiyo Tarehe 19 Machi,2018  katika nyumba anayoishi.
Aidha Parangyo ameiambia mahakama kuwa mwananchi haruhusiwi kumiliki risasi au silaha ya kivita kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi ya Tanzania.
Mmoja wa mashuhuda upande wa washtaki akiwemo Mwenyekiti wa kijiji cha Kambuzi Halt Bw.Tuamin Elly,Bw.Huba alikuwa akilalamikikiwa na wananchi kwa kujihusisha na matukio ya uhalifu mara kwa mara.
Hata hivyo mtuhumiwa amekana mashtaka dhidi yake ya kumiliki risasi hizo bila kibali.
Aidha ameiomba mahakama impunguzie adhabu atakapobainika kuwa na hatia kwa kuwa anategemewa na familia yake pamoja na mama yake mzazi ambaye kwa sasa ni mgonjwa akimtegemea pia.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA