Posts

Showing posts from January 14, 2018

MBUNGE CHADEMA MKOANI KATAVI AIBUKA NA HOJA YA KUPATIKANA DIWANI MWINGINE WA KATUMBA

Image
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi kupitia   Chadema Rhoda Kunchela amesema kitendo   cha kata ya Katumba halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi kutokuwa na diwani ni kuchelewesha maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo. Hayo yamebainishwa leo na Mbunge huyo na kusema kuwa wananchi wanakosa uwakilishi  na kushauri uchaguzi ufanyike ili apatakane diwani mwingine. Katika hatua nyingine Mh Kunchela  amezungumzia ziara aliyoifanya mwenyekiti wa Bawacha taifa  Halima Mdee amabye pia ni mbunge wa jimbo la kawe na kusema ziara  hiyo imefanyika mkoani katavi ikilenga kuimarisha uhai wa chama hicho. Diwani aliyekuwa akiongoza kata hiyo Mh Seneta Baraka mwezi Novemba mwaka jana alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kupokea rushwa. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS WA LIBERIA ATIMULIWA

Image
Rais anayemaliza muda wake nchini Liberia,Ellen Johnson Sirleaf,ametimuliwa katika chama chake kwa tuhuma za kutomuunga mkono mgombea wake ili amrithi. Chama chake cha Unity kinamtuhumu Bi.Ellen, kwa kuwahamasisha wananchi kutompigia kura mgombea ambaye alikuwa Makamu wa Rais Joseph Boakai. Aidha,chama hicho kinamtuhumu kwa kukiuka Katiba kwa madai ya kumfanyia kampeni George Weah,ambaye aligombea kupitia chama cha Coalition for Democratic Change na kuibuka mshindi. Bw.Weah ambaye ni mwanasoka nyota wa zamani, anatarajiwa kuapishwa rasmi Januari 22 mwaka huu ikiwa ni mara ya kwanza Liberia kushuhudia mabadiliko ya uongozi kwa njia ya amani tangu mwaka 1944. Chanzo:EATV Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME AFANYA ZIARA HAPOA NCHINI,APANGA MIKAKATI YA MAENDELEO NA RAIS MAGUFULI

Image
Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mhe.Paul Kagame leo tarehe 14 Januari, 2018 amefanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli. Katika Picha Rais Magufuli Kushoto na Kulia ni Rais Kagame Mhe. Rais Kagame amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Mhe.Rais Magufuli na kisha kulakiwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, na baadaye akaelekea Ikulu ambako pamoja na kufanya mazungumzo ya faragha, viongozi hao wamezungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari. Mhe.Rais Magufuli amesema katika mazungumzo yao wamekubaliana ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kati ya Isaka nchini Tanzania na Kigali nchini Rwanda yenye urefu wa takribani kilometa 400 uanze mwaka huu (2018), na wamewaagiza Mawaziri wanaohusika na miundombinu kukutana ndani ya kipindi cha wiki mbili kuanza sasa il

MELI YA MAFUTA ILIYOKUWA IKITEKETEA MOTO IMEZAMA BAHARINI

Image
Meli ya mafuta ambayo imekuwa ikiteketea kusini mwa bahari ya China kwa zaidi ya wiki moja hatimaye imezana Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Meli ya mafuta iliyokuwa ikiteketea moto imezama baharini . Kwa mjibu wa vyombo vya habari vya China,Sanchi na meli nyingine ya mizigo ziligongana kilomita 260 nje ya Shanghai Januari 6 mwaka huu ambapo baadaye ilianza kusombwa kusini mashariki kwenda Japan. Maafisa wa Iran sasa wanasema  Image caption Meli hiyo ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta lakini maafisa wanasema kuwa hakuna hatari kubw a.  wahudumu wote 32, wakiwemo raia 30 wa Iran na wawili raia wa Bangladesh wote walifariki. Meli hiyo ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta lakini maafisa wanasema kuwa hakuna hatari kubwa ambapo Meli zingine 13 na kikosi kutoka Iran wamekuwa wakishiriki katika jitihada za kuokoa licha ya kuwepo hali mbaya ya hewa. Siku ya Jumamosi wafanyakazi walikuwa wameingia kwenye meli hiyo ambapo walipata miili ya wahudumu wawili ndani ya