MBUNGE CHADEMA MKOANI KATAVI AIBUKA NA HOJA YA KUPATIKANA DIWANI MWINGINE WA KATUMBA

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi kupitia  Chadema Rhoda Kunchela amesema kitendo  cha kata ya Katumba halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi kutokuwa na diwani ni kuchelewesha maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo.
Hayo yamebainishwa leo na Mbunge huyo na kusema kuwa wananchi wanakosa uwakilishi  na kushauri uchaguzi ufanyike ili apatakane diwani mwingine.
Katika hatua nyingine Mh Kunchela  amezungumzia ziara aliyoifanya mwenyekiti wa Bawacha taifa  Halima Mdee amabye pia ni mbunge wa jimbo la kawe na kusema ziara  hiyo imefanyika mkoani katavi ikilenga kuimarisha uhai wa chama hicho.
Diwani aliyekuwa akiongoza kata hiyo Mh Seneta Baraka mwezi Novemba mwaka jana alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kupokea rushwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA