RAIS WA LIBERIA ATIMULIWA

Rais anayemaliza muda wake nchini Liberia,Ellen Johnson Sirleaf,ametimuliwa katika chama chake kwa tuhuma za kutomuunga mkono mgombea wake ili amrithi.
Chama chake cha Unity kinamtuhumu Bi.Ellen, kwa kuwahamasisha wananchi kutompigia kura mgombea ambaye alikuwa Makamu wa Rais Joseph Boakai.
Aidha,chama hicho kinamtuhumu kwa kukiuka Katiba kwa madai ya kumfanyia kampeni George Weah,ambaye aligombea kupitia chama cha Coalition for Democratic Change na kuibuka mshindi.
Bw.Weah ambaye ni mwanasoka nyota wa zamani, anatarajiwa kuapishwa rasmi Januari 22 mwaka huu ikiwa ni mara ya kwanza Liberia kushuhudia mabadiliko ya uongozi kwa njia ya amani tangu mwaka 1944.
Chanzo:EATV

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA