Posts

Showing posts from 2016

GEREZA LA KALILANKULUKULU NA TAASISI ZAKE AMBAZO NI SHULE NA ZAHANATI HATARINI,BAADHI YA WAFUNGWA HAWANA SARE,BAADHI YA ASKARI MAGEREZA NAO WALAZIMIKA KUTUMIA PESA ZAO KUSHONA SARE KWA MIAKA 8 SASA,KUTA ZA MAJENGO YA ZAHANATI NAYO KUANGUKA MUDA WOWOTE,VYOO VYA WANAFUNZI NAVYO VYAJAA VYAZIBA BILA HATUA KUCHUKULIWA KIPINDUPINDU KUBISHA HODI.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika Katavi GEREZA la Kalilankulukulu lililopo Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi lililoanzishwa mwaka 1973 ,linakabiliwa na matatizo mbalimbali yakiwemo baadhi ya wafungwa wa gereza hilo kukosa sare huku pia baadhi ya asakari wa gereza hilo,wakilazimika kutumia pesa yao kushona sare zao kutokana na serikali kutowapa sare hizo tangu mwaka 2009 licha ya viongozi kadhaa wa wizara,Mkoa hadi Wilaya kuwa na taarifa ya matatizo hayo.   Mwigulu Nchemba waziri wa mambo ya ndani ya Nchi ambaye kwa kiasi kikubwa gereza zipo chini ya wizara yake kama waziri                                                                Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe Naibu waziri wa Nishati na madini(Mbunge wa Jimbo la Katavi)                       

JIMBO LA MPANDA MJINI LAPATA MGAO WA MADAWATI 537 KUTOKA MFUKO WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda JIMBO la Mpanda mjini Mkoani Katavi limepatiwa mgao wa madawati 537 kutoka mfuko wa ofisi ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2017 MWENGE KUWASHWA MKOANI KATAVI KUZIMIWA ZANZIBAR

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama UZINDUZI wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2017 unatarajia kufanyika Mkoani KATAVI na kilele cha mbio za mwenge huo kitafanyika Zanzibar.                                                  

TANZANIA NA UHORANZI ZASAINIANA MKATABA WA KUWEKA UMEME WA UHAKIKA MKOANI KATAVI,ZAIDI YA VIJIJI 15 KUNUFAIKA

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi SERIKALI za Tanzania na Uhoranzi kwa pamoja zimesainiana Mkataba wa Shilingi Bilioni 44/= ili kufanikisha ukamilika kwa mradi wa umeme wa uhakika Mkoani Katavi ifikapo mwezi Juni mwaka 2017. Mashine zinazofua umeme                                  

MANISPAA YA MPANDA BADO IMESHINDWA KULIPA SHILINGI MILIONI 321 KWA WAZABUNI WALIOJENGA MAABARA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA MANISPAA.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi HALMASHAURI ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imesema bado haina uwezo wa kulipa Shilingi Milioni 321 inayodaiwa za wazabuni waliojenga maabara katika Shule Mbalimbali za Manispaa ya Mpanda. Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Francis Nzungu(PICHA NA.Issack Gerald)   Katika picha ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Ofisi Za Hamlshauri ya Manispaa ya Mpanda na pia ndipo ulipoUkumbi  wa Mikutano wa Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald)                                    

MKUU WA WILAYA MPANDA AWAAGIZA WATUMISHI WENYE VYETI BANDIA KUJIONDOA WENYEWE KABLA YA KUKAMATWA,MANISPAA YA MPANDA NAYO YAAGIZWA KUWA NA NIDHAMU YA MATUMIZI YA BAJETI YA FEDHA ZA MAENDELEO.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi. Lilian Charles Matinga,amewaagiza watumishi wote wenye vyeti bandia Wilayani Mpanda kujiondoa wenyewe kwa hiari kabla ya kukamatwa na hatua kali kuchukuliwa dhidi yao. MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Charles Matinga(Asiyevaa wigi) Mh.Sebastian Mwakabafu Diwani wa kata ya uwanja wa ndege katika kikao akiuliza swali                                

MUWASA : WAKAZI MANISPAA YA MPANDA WANAKOSA MAJI KUTOKANA NA UPUNGUFU WA MAJI KUTOKA VYANZO VYA MAJI

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi MAMLAKA ya maji safi na salama Manispaa ya Mpanda MUWASA Mkoani Katavi imesema kuwa,tatizo la upatikanaji wa maji lililopo kwa sasa kwa wakazi wa Manispaa ya Mpanda,linatokana na upungufu wa kina cha maji katika vyanzo vinavyotoa maji. Ikorongo Namba 2 chanzo cha Maji Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald)                                 

VIJANA UVCCM MKOANI KATAVI WAJITOKEZA KUCHANGIA DAMU SALAMA HOSIPTALI YA WILAYA YA MPANDA

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama –Mpanda Katavi VIJANA WA UMOJA wa chama cha Mapinduzi UVCCM Mkoani Katavi,leo wamejitokeza kuchangia damu salama katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.

KUHUSU KATAVI NA SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI LEO OKTOBA 11,2016-P5 TANZANIA INAKUSOGEZEA

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Katavi ZAIDI ya makosa 100 ya unyanyasaji kwa mtoto wa kike yameripotiwa katika kipindi cha miezi 9 iliyopita ikiwa ni pamoja na makosa ya ubakaji,kutupa watoto,kuwapa mimba wanafunzi na kuwaachisha masomo.

BARAZA LA MADIWANI WILAYANI TANGANYIKA LAIOMBA SERIKALI KUKAMILISHA MIRADI VIPORO YA MAENDELEO ILI WANANCHI KUENDELEA KUWA NA IMANI NA SERIKALI.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama –Tanganyika Katavi BARAZA la madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,limeiomba serikali kuhakikisha inakamilisha miradi ya maendeleo katika kata mbalimbali ili kuwanufaisha wananchi kiuchumi na kimaendeleo. Madiwani wa Baraza la madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda wakiwa katika kikao(PICHA NA.Issack Gerald) Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Hamad Hassan Mapengo(PICHA NA.Issack Gerald)                                                           

SHIRIKA LA UNHCR LAKABIDHI GARI LA SHILINGI MILIONI 150 KWA JESHI LA POLISI WILAYANI TANGANYIKA,WAAHIDI KUTOA MAFUTA NA KULIKARABATI LINAPOHARIBIKA,JESHI LA POLISI KATAVI LAAGIZWA KUIMARISHA USALAMA.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama- Katavi SHIRIKA la Wakimbizi duniani UNHCR limekabidhi gari mpya kwa jeshi la Polisi Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,ili kurahisisha na kuongeza utendaji kazi wa jeshi hilo katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao. Picha ya Pamoja ya Jeshi la Polisi Baada ya UNHCR kukabidhi gari kwa Jeshi La Polisi Wilayani Tanganyika(PICHNA NA.Issack Gerald),wa Kwanza kutoka kulia ni kamanda wa Jeshi Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda                                

LEO NI SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI MAADHIMISHO KITAIF AKUFANYIKA SHINYANGA,MIKOA 21 INAONGOZA KWA MIMBA ZA UTOTONI KINARA NI SHINYANGA KWA ASILIMIA 59.

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama LEO ni siku ya mtoto wa kike duniani ambapo siku hiyo kitaifa inaadhimishwa Mkoani Shinyanga.

WASAFIRI KUTOKA KATAVI,TABORA NA KIGOMA WANAOTUMIA TRENI YA RELI YA KATI KUONGEZEWA BEHEWA KURAHISISHA USAFIRI

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama- Katavi SERIKALI imewahakikishia wakazi wa mikoa ya Katavi,Tabora na Kigoma kuwa itaongeza mabehewa ya abiria na mizingo katika treni ya reli ya kati ili kuruhusu abiria wengi kusafiri na kusafirisha   mizigo yao kuwa wasafiri wengi wanatumia usafiri wa treni.                                               

BARAZA LA MADIWANI HALMSHAURI YA WILAYA YA MPANDA KUFANYA KIKAO CHAKE KESHO,SHILINGI MIL.120 ZILIZOTUMIKA KINYUME NA MALENGO,BARAZA LA MADIWANI KUTOA TAMKO

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi BARAZA la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,kesho linatarajia kufanya kikao chake cha robo ya mwaka kwa mwaka 2016 ambapo masuala mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo kutoa   tamko la kubadilishwa matumizi ya Shilingi milioni 120 zilizokuwa zitumike kununulia gari la Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri hiyo ambapo zilitumika kwa ajili ya Masuala ya mitihani. Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mh.Hamad Hassan Mapengo(PICHA NA.Issack Gerald)                                                 

SHIRIKA LA UNHCR KESHO KUKABIDHI GARI KWA JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI KUSAIDIA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi SHIRIKA la wakimbizi duniani UHNCR Mkoani Katavi,kesho linatarajia kukabidhi gari kwa jeshi la Polisi Mkoani Katavi ili kurahisisha shughuli za ulinzi na usalama za jeshi hilo.                                           

WALEMAVU WASIOONA 127 WAKIWEMO WANAFUNZI 58 MKOANI KATAVI BADO WANA MATATIZO MAKUBWA YA KUKOSA HUDUMA STAHIKI KATIKA ELIMU NA AFYA

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Katavi CHAMA cha Wasioona Tanzania TLB Mkoani Katavi,kimesema Walemavu zaidi ya 127 wasioona waliopo Mkoani Katavi,bado wanakabiliwa na hatari ya kukosa huduma muhimu mbalimbali kama elimu,afya na mengineyo muhimu kutokana na jamii kuendelea kuwa na mtazamo kuwa,walemavu hawana mchango wa kuleta maendeleo. Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Tulia Akson akihutubia siku ya fimbo nyeupe Mkoani Mbeya akiwa ndiye Mgeni rasmi(PICHA NA.Issack Gerald) Bw.Emmanuel Simon katibu wa TLB taifa akiwasilisha taarifa wakati wa maadhimisho ya siku ya wasioona maarufu siku ya fimbo nyeupe Mkoani Mbeya(PICHA NA.Issack Gerald)                              

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AVUNJA BODI YA CHAMA WAKULIMA WA TUMBAKU MISHAMO TAMCOS

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika MKUU wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Saleh Mbwana Mhando,ameivunja bodi ya chama cha wakulima cha tumbaku MISHAMO TAMCOS na kuamru viongozi wote wa bodi hiyo wakamatwe haraka.                                              Wakulima wa Chama cha Ushirika Mishamo Tamcos katika picha wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika pichani hayupo Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Mhando akizungumza na wakulima wa chama cha Ushirika MISHAMO TAMCOS(Picha na Issack Gerald) Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha MISHAMO TAMCOS Bw. Bw.Pridas Amakredo(picha na Issack Gerald)

MKUU WA MKOA WA KATAVI APOKEA SHILINGI 500,000/= KUTOKA MUKABUBINGA KWA AJILI WAATHIRIKA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA,FEDHA ILIYOCHANGWA YAFIKIA MIL. 13,344,600 KUWASILISHWA KAGERA JUMATATU.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo - Katavi MKUU wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral mstaafu Raphael Muhuga amepokea Shilingi laki tano kutoka kwa MUKABUBINGA ambao ni Umoja wa wanakagera waishio Wilayani Mpanda ambapo fedha hiyo ni kwa ajili ya kuwachangia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga(PICHA NA.Issack Gerald)                    

TCCIA KATAVI : SERIKALI ITAFUTE MFUMO WA KUDUMU KUSIMAMIA SEKTA YA KILIMO,MENEJA MPANDA KATI NAYE ASEMA UZALISHAJI WA TUMBAKU UMEPUNGUA KUTOKA KILO 3.5 - 1.4 MILIONI

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi CHAMA cha watu wenye kilimo,viwanda na Biashara TCCIA Mkoani Katavi,kimeishauri serikali kutafuta mfumo wa kudumu utakaosimamia sekta ya kilimo ikiwemo kusimamia mfumo wa usambazaji wa pembejeo za kilimo hapa nchini ili wakulima walime kilimo chenye tija kwao kutokana na matumizi sahihi ya pembejeo hizo ikiwa zitaletwa kwa wakati.                                             

ASILIMIA 45 YA WATOTO CHINI YA MIAKA 18 TANZANIA HUPATA UJAUZITO NA KUPOTEZA MAISHA WAKATI WA KUJIFUNGUA

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama -Nkasi Rukwa Asilimia 45 ya watoto wa kike waliochini ya  umri wa miaka 18 hupata ujauzito na kupoteza maisha kila mwaka  wakati wa kujifungua kwa mjibu wa  utafiti uliofanywa  na Shirika lisilokuwa la kiseriklai la Plan International Tanzania.

MFAHAMU PROFESA LIPUMBA WA CHAMA CHA CUF

Image
IBRAHIM HARUNA LIPUMBA (amezaliwa tar. 6 Juni 1952 , Ilolangulu , Tabora , Tanzania ) ni mwanasiasa nchini Tanzania na pia mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Civic United Front (CUF - Chama Cha Wananchi) ambaye kawa sasa chama cha CUF kimetangaza kumfuta katika chama hicho. Prof Ibrahim Haruna  Lipumba                                               

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI KUFANYIKA LEO 1/10/2016

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, imesema   leo inaadhimisha kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.

UKOSEFU WA FEDHA,WAZEE KATAVI WASHINDWA KUHUDHURIA MAADHIMISHO YA KESHO SIKU YA WAZEE DUNIANI YATAKAYOFANYIKA MKOANI MBEYA

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo mashama-Katavi UMOJA wa wazee Mkoani Katavi umeshindwa kupeleka wawakilishi katika maadhimisho ya Siku ya wazee Duniani yanayotarajiwa kufanyika kitaifa kesho Mkoani Mbeya. Moja ya mikitano iliyokuwa ikijadili maslahi ya wazee(PICHA NA Issack Gerald )Septemba 2014                                            

MATATIZO MENGI BADO SOKO KUU LA WILAYA YA MPANDA

NA.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika Katavi SOKO kuu la Mpanda,mkoani Katavi linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo msongamano wa wafanyabiashara, mpangilio holela na ukosefu wa taa za kusaidia ulinzi.

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AONGOZA HARAMBEE KUWACHANGIA WAATHIRIKA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA SHILINGI MIL.4,656,500 ZAPATIKANA.

Image
NA.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika Katavi MKUU wa Wlaya ya Tanganyika Bw.Saleh Mbwana Mhando ameongoza harambee ya kuwachangia waathirika wa tetetmeko la ardhi Mkoani Kagera ambapo Shilingi MIL.4,656,500/=zimepatikana ambapo kati ya hizo shilingi MIL.4,416,000/= ni fedha taslimu.                                                                               

MWALIMU WILAYANI MLELE AHUKUMIWA JELA MIAKA 30 KWA KUSABABISHA UJAUZITO KWA MWANAFUNZI WAKE

Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi MAHAKAMA ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imemhukumu Mwalimu wa Shule ya Msingi Ukingwamizi, Une Thom kutumikia kifungo cha miaka 32 jela.

TANESCO NA UFAFANUZI WA TATIZO LA UMEME MPANDA KATAVI

Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi Uchakavu na ubovu wa mitambo ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa katavi ndiyo imeelezwa kuwa ndio chanzo kinachosababisha kutokuwa na umeme wa uhakika. Meneja mahusiano wa

MKUU WA WILAYA YA MPANDA AHAMASISHA HARAMBEE KUWACHANGIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama- Mpanda Katavi MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi. Lilian Charles Matinga,ametoa wito kwa wakazi wa Wilaya ya Mpanda kujitokeza kwa hiari katika harambee ya kuwachangia wakazi wa Mkoa wa Kagera walioathiriwa wa tetemeko la ardhi Septyemba 10 mwaka huu.

KAMATI TENDAJI MRADI ELIMU JUMUISHI MKOANI KATAVI NA UJUMBE WA UGENI KUTOKA MIKOANI WAFANYA KIKAO KUJADILI MAHITAJI YA WATOTO WENYE ULEMAVU

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Katavi JAMII Mkoani Katavi imetakiwa kushiriki ipasavyo kuwafichua watoto wenye Ulemavu ili wapatiwe elimu kama watoto wengine wasio na ulemavu.

KUTOKA WILAYANI MLELE KATAVI -TUKIO LA NYUMBA KUCHOMWA MOTO

Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama –Mlele Katavi NYUMBA za wakazi ambazo idadi yake haijafahamika eneo la Namba moja lililopo Kata na Tarafa ya Inyonga Wilayani Mlele Mkoani Katavi,leo zimeteketezwa kwa moto na baadhi ya mali zilizokuwemo kuteketezwa katika nyumba hizo. Kwa mjibu wa baadhi ya wakazi ambao mali zao zimeteketea ,wakizungumza na Mpanda Radio Kwa njia ya Simu kwa masikitiko makubwa akiwemo Bi.Tatu M asanja wamesema kuwa, tukio hilo ambalo wameliita la kushtukiza asubuhi ya leo,wamedai limetekelezwa na askari Mkoani Katavi kuanzia majira ya asubuhi. Wametaja baadhi ya mali zao ambazo zimechomwa kwa moto mbali na nyumba zao kuwa ni pamoja na Vyakula na mavazi huku watoto wakizagaa ovyo katika eneo hilo bila wazazi wao baada ya wazazi kukimbilia kusikojulikana kufuatia wengine kupigwa na askari hao. Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP damasi Nyanda,akizungumza na Mpanda Radio Kwa njia ya Simu mchana wa leo,amesema hajapata taarifa ya utekelezwaji wa

KUHUSU SIKU YA AMANI DUNIANI,WAKAZI MKOANI KATAVI WASEMA HIKI

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Katavi BAADHI ya wakazi Mkoani Katavi,wameshauri siku ya amani duniani itumike kutafakari namna ya kudumisha amani iliyopo hapa nchini.                                   

TAASISI YA TWAWEZA WAENDESHA KONGAMANO LA WADAU WA ELIMU MPANDA,WAZAZI WALEZI WATAKIWA KUTAMBUA UMUHIMU WA ELIMU KWA WATOTO

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi WAZAZI na WALEZI katika manispaa ya Mpanda Mkoani wameshauri jamii kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto ikiwa ni urithi kwa maisha bora. Wanafunzi mkoani Katavi                                                

NYUMBA ILIYOTEKETEA KWA MOTO JUZI ,CHUMBA CHA MPANGAJI HASARA NI ZAIDI YA MILIONI MOJA NA LAKI TANO(1,500,000).

Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda Imebainika kuwa janga la moto lililotokea juzi katika Mtaa wa Mpadeco Kata ya Mkananyagio Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,umesababisha Bi.Grace Emmanuel Mkazi wa mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio kupata hasara ya Zaidi ya Shilingi Miloni moja na laki tano (1,500 ,000). B.Grace amesema Moto huo uliozuka mchana uliunguza Vitanda 2 vyenye thamani ya laki tano na elfu sitini(560,000),Magodoro mawili 5 kwa 6 yenye thamani ya Shilingi laki tatu(300,000),Maguni ya Mpunga 4 thamani yake zaidi ya Shilingi laki 2(200,000),Upotevu wa fedha taslimu Shilingi laki nne na nusu za mkopo zilizopotea wakati wa uokozi na nguo ambazo tahamani yake haijafahamika. Akizungumza akiwa nyumbani kwake muda mfupi baada ya kutoka hospitali ya Wilaya ya Mpanda,alikolazwa baada ya kuzimia kutokana mshtuko alioupata baada ya kupata hasara hiyo,amesema kuwa hata hivyo hajatambua kiasi alichotumia kwa ajili ya matibabu. Hata hivyo amekwishafungua jarada Polisi ili ili kufany

NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO MPANDA

Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda Moto umeunguza nyumba ya Familia moja na kusababisha hasara ya mali ambayo thamani yake haijajulikana katika mtaa wa Migazini kata ya Makanyagio   Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

MKUU WA WILAYA TANGANYIKA:ENEO LA LUHAFE SASA KUJENGWA MJI WA MAKAZI NA BIASHARA.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando,ametangaza wakazi wa eneo la Luhafe lililopo kata ya Majalila,kulitumia eneo hilo kwa makazi na shughuli za kibiashara baada ya mgogoro wa uhalali wa eneo hilo wa muda mrefu. Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Saleh Mbwana Mhando akihutubia wakazi wa kitongoji cha Luhafe(PICHA NA.Issack Gerald)Septemba 16,2016                                                                           

VIJIJI ZAIDI YA 14 VYA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO KUPATA UMEME WA REA AWAMU YA III MWAKA 2016

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda,Katavi Meneja wa TANESCO mkoa wa Katavi Mhandisi Julius Sabu amesema katika awamu ya tatu ya umeme wa REA wanampango wa kusambaza umeme katika vijiji ambavyo havikupitiwa na mpango huo katika awamu zilizopita.                                    

WAKAZI WILAYANI TANGANYIKA WAAGIZWA KUONGEZA KASI YA KUJENGA SEKONDARI KILA KATA

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika WAKAZI wilayani Tanganyika Mkoani Katavi kwa Kushirikiana na uongozi wa vijiji na kata   katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,wameagizwa kuweka mikakati ya ujenzi wa shule za Sekondari kila kata ,ili kila mwanafunzi asome bila kuhangaika na badala yake apate elimu bora.                                       Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Mhando akishiriki ujenzi Shule ya sekondari ya Bulamata  kata ya Bulamata(PICHA NA Issack Gerald)Septemba 16,2016                                          Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika akizungumza na wananchi eneo la kijiji cha Busongola kunakojengwa Shule ya Sekondari Bulamata(PICHA NA.Issack Gerald) Septemba 16,2016                                                       Wananchi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Isubangala kijiji cha Isubangala kata ya Ilangu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya(hayupo pichani)(PICHA NA.iSSACK gERALD) Septemba 16,2016

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AAGIZA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 200 ZA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU CHAMA CHA USHIRIKA TAMCOS KULIPWA NDANI YA SIKU 15.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Bw.Saleh Mbwana Mhando,ameuagiza uongozi wa bodi ya Chama cha Msingi cha Ushirika TAMCOS na Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Luxford Mbunda,kuhakikisha wanalipa   zaidi ya Shilingi milioni 200 wanazodai wakulima wa zao la tumbaku wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kwa misimu 3 ya kilimo kuanzia mwaka 2011-2015 kabla ya Septemba 30 mwaka huu. Baadhi ya Wakulima wa Zao la Tumbaku wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika(hayupo pichani) katika Ofisi za TAMCOS Mishamo(PICHA NA.Issack Gerald) Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Mhando Aliyesimama akihutubia wakulima wa tumbaku wa chama cha Msingi cha Ushirika TAMCOS Mishamo(PICHA NA.Issack Gerald)                                       Wakulima wa chama cha Msingi cha Ushirika TAMCOS Mishamo wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika(hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika Septemba 15,2016 kati

KIFO CHA MTU KUJINYONGA KATAVI,NDUGU,MASHUHUDA WASIKITIKA

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi MTU mmoja anaekadiliwa kuwa na umri wa miaka 30 Innocent Milambo mkazi wa mtaa wa kigoma kata ya Makanyagio wilayani Mpanda   mkoani Katavi,amekutwa amekufa kwa kujinyonga   usiku wa kuamkia leo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda(PICHA NA.Issack Gerald)                                                             

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA ATOA AGIZO KWA WATUMISHI WA WILAYA HIYO,ATAKA WAFANYE KAZI KWA WELEDI KWA MANUFAA YA WANANCHI NA KUIEPUKA RUSHWA.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika Katavi MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Saleh Mbwana Mhando,amewaagiza watumishi wa umma Wilayani Tanganyika,kufanya kazi kwa weledi na kasi ili kufikia maendeleo yanayohitajika kwa wananchi. Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika(Mwenye tai) akiwa na baadhi ya watumishi wa Wilaya hiyo baada ya kikao(PICHA NA.Issack Gerald)Septemba 14,2016 Baadhi ya watumishi wa idara mbalimbali halmashauri ya wilaya ya Tanganyika katika kikao cha utumishi na mkuu wa Wilaya(Hayupo pichani)(PICHA NA.Issack Gerald)Septemba 14,2016                                           

MIFUGO KUZAGAA MITAANI KWAPIGWA WILAYANI KIBONDO

Na.Mwandishi wetu- Jastini Cosmas-Kibondo Kigoma HALMASHAURI ya wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma,imewaagiza wananchi katika Halmshauri hiyo kutoachia mifugo yao ovyo katika kipindi hiki cha msimu wa kilimo,kutokana na mifugo hiyo kuwa waharibifu wa mazao.

KINACHOIGUSA MIKOA YA KATAVI,RUKWA NA KIGOMA KUTOKA VIKAO VYA BUNGENI DODOMA LEO SEPTEMBA 8,2016

Image
Na.Issack Gerald-Dodoma Serikali imesema,inaendelea kuweka mikakati ya kuwa na kiwanda cha kutengeneza pikipiki za bodaboda ili kuwajengea vijana kuwa na uwezo wa kununua pikipiki zao,kuliko kuendelea kuwatumikia matajiri wenye uwezo wa kumiliki pikipiki hizo. Wabunge wakiwa bungeni Mjini Dodoma leo Septemba 8,2016                                   

KUMEKUCHA BUNGENI TENA ,MISWADA 6 UKIWEMO WA HABARI KUWASILISHWA,WABUNGE WA UPINZANI MGUU SAWA BUNGENI

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo MKUTANO wa Nne wa Bunge la 11 unatarajiwa kuanza leo mjini Dodoma, huku miswada sita ukiwemo wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari ukitarajiwa kuchukua nafasi kubwa.  

RPC KATAVI : JESHI LA POLISI LIMEJIANDAA KUWADHIBITI WAANDAMANAJI OPARESHENI UKUTA,VYAMA VILIVYOKUWA VIMEPANGA KUANDAMANA VYAAHIRISHA MAANDAMANO

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi JESHI la Polisi Mkoani Katavi lilikuwa limesema limefanya maandalizi ya kutosha kuwadhibiti watu,kikundi au vyama vya siasa ambavyo vingefanya maandamano kesho Septemba mosi. Viongozi wa upinzani wakati wa kikao na wanahabari Dar es Salaam ACP Damasi Nyanda Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald)Agosti 31,2016                                           

RPC NYANDA KATAVI LEO KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAANDAMANO YA OPARESHENI UKUTA SEPTEMBA MOSI.

Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi KAMANDA wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ASP Damasi Nyanda leo anatarajia kukutana na waandishi wa habari Mkoani Katavi kuzungumzia mandamano ya Opareshen Ukuta yanayoratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

WAFANYABIASAHARA MANISPAA YA MPANDA WAPEWA SIKU 6 KUONDOKA MASOKO YASIYO RASMI KABLA YA NGUVU KUTUMIKA.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda WANANCHI wanaofanya biashara katika masoko yasiyo rasmi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wametakiwa kuondoka na bidhaa zao wenyewe kwa hiari kabla ya Septemba 5 mwaka huu kuondolewa kwa nguvu. Katika Picha Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu(PICHA NA.Issack Gerald) Miongoni mwa wafanyabishara wanaopigwa marufuku soko lisilo rasmi lililopo Ujenzi Machinjioni Mpanda hotel.                                                    

MKUU WA WILAYA TANGANYIKA AONYA WATAKAOANDAMANA OPARESHENI UKUTA SEPTEMBA MOSI,ASEMA OPARESHENI UKUTA IWE NI KUJENGA MADARASA,KUTENGENEZA MADAWATI NA SHUGHULI NYINGINE ZA MAENDELEO.

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Saleh Mbwana Mhando,ametoa onyo kwa wananchi na wanachama wa vyama vya siasa watakaofanya maandamano ya Opareshen Ukuta katika Wilaya hiyo yanayotarajia kuanza Septemba mosi.  Mkuu wa Wilaya ya Tanganyiika Saleh Mhando                                        

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AKAZA MWENDO KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA WILAYA YAKE

Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh.Saleh Muhando ameahidi kulishughulikia swala la mgogoro wa ardhi katika eneo la Lyamgoroka eneo ambalo linaonekana kuwa limeuzwa na   mwenyekiti wa kijiji hicho    kinyume cha sheria ya ardhi.

WANAUME WATAJWA KUWA MIONGONI MWA SABABU ZINAZOCHANGIA KUONGEZEKA VVU KATAVI

  Na.Richard Sokoni-Mpanda Imebainika kuwa   ongezeko la   maambukizi ya virus vya ukimwi (VVU) kunatokana   na   baadhi ya mwanaume   kutojitokeza kupima afya zao sanjari na wenzi wao .

VIJANA WATII AGIZO LA MKURUGENZI WA MANISPAA KUTOSAFISHA VYOMBO VYA USAFIRI KATIKA VYANZO VYA MAJI

Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda Vijana na watu waliokuwa wakitumia mto Mpanda eneo la daraja linalotenganisha Kata ya Mpanda Hotel na Misunkumilo kusafisha magari na vyombo vingine vya usafiri,wamesitisha shughuli hiyo kutii agizo la mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda akiwataka kutofanya shughul hiyo kwa lengo la kulinda vyanzo vya maji.

JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI WAFANYA MAZOEZI KUPAMBANA NA UHARIFU,WANANCHI MITAANI WAKUMBWA NA TAHARUKI.

Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi JESHI la Polisi Mkoani Katavi limetoa onyo kwa watu watakaosababisha ukosefu wa amani katika Mkoa wa Katavi likisema kuwa halitawafumbia macho watu hao na badala yake Jeshi hilo litachukua hatua kali za kisheria kukomesha vitendo vya uharifu.

TRA RUKWA NA KATAVI YAENDESHA SEMINA KUHUSU MFUMO MPYA ULIPAJI KODI

Image
Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda WAFANYABIASAHARA mikoa ya Rukwa na Katavi wametakiwa kutofumbia macho vikwazo vinavyotokana na mfumo mpya wa ulipaji kodi na badala yake watoe taarifa na maoni ili kuangalia kama kuna uwezekano wa kuondoa vikwazo hivyo ili wafanye biashara zao kwa uhuru.