TCCIA KATAVI : SERIKALI ITAFUTE MFUMO WA KUDUMU KUSIMAMIA SEKTA YA KILIMO,MENEJA MPANDA KATI NAYE ASEMA UZALISHAJI WA TUMBAKU UMEPUNGUA KUTOKA KILO 3.5 - 1.4 MILIONI



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
CHAMA cha watu wenye kilimo,viwanda na Biashara TCCIA Mkoani Katavi,kimeishauri serikali kutafuta mfumo wa kudumu utakaosimamia sekta ya kilimo ikiwemo kusimamia mfumo wa usambazaji wa pembejeo za kilimo hapa nchini ili wakulima walime kilimo chenye tija kwao kutokana na matumizi sahihi ya pembejeo hizo ikiwa zitaletwa kwa wakati.
                                            

Ushauri huo umetolewa na Katibu mtendaji wa chama cha watu wenye viwanda ,kilimo na biashara Mkoani Askofu  Raban Ndimubenya katika mahpjiano na waandishi wa habari Ofisini Kwake kuhusu nafasi ya  TCCIA katika kusaidia wakulima kutatua changamoto za kilimo zinazowakabili ikiwemo matatizo ya pembejeo na masoko ya kuuzia mazao.
Askofu Ndimubenya pia amesema kuwa wakulima wa tumbaku hawajaingizwa katika chama cha TCCIA na amesema wakulima wa zao la tumbaku watakaotaka kujiunga na TCCIA Mkoani Katavi watapatiwa nafasi.
Katika hatua nyingine,ikiwa msimu wa kilimo cha zao la tumbaku ndiyo umewadia,kwa upande wake Meneja wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Mpanda Kati Bw Amani Rajabu ametoa wito kwa wakulima wa zao la tumbaku kulima zao hilo kwa kiwango cha shamba atakaloweza kulitunza na kupata mapato mengi kuliko kulima shamba kubwa na kushindwa kulitunza na kuambulia mapato kidogo tena isiyo na ubora.
Aidha Bw.Rajabu amesema,uwezo mdogo wa makampuni yanayonunua tumbaku mkoani Katavi wakati wakulima wakiwa na uwezo mkubwa wa kulima tumbaku,kunawaathiri wakulima kiuchumi kwa kuwa wana uwezo wa kulima zaidi ya kiwango kinachohitajika katika kampuni katika manunuzi.
Wakati huo huo Bw.Rajab amesema kutokana uwezo mdogo wa kampuni kununua  tumbaku kiwango cha uzalishaji kwa wakulima wa zao hiloika chama cha Msingi cha Ushirika Mpanda Kati kimeshuka kutoka zaidi ya kilo milioni 3.5 hadi kufikia kilo milioni 1.4.
Awali kabla ya chama cha msingi cha ushirika Mpanda Kati kilipokuwa hakijagawanywa mwaka 2014 na kupata usajili mpya,kilikuwa na vijiji 17 vilivyokuwa wanachama ambapo kwa sasa kuna vijiji 11 ambavyo ni Igagala,Ifukutwa ,Majalila,Mpembe,Igalula,Mchaka,Mpolwe,Katonyaga,Milala Shongo,Ngomalusambo,na Kabungu.
Hata hivyo bado wakulima Mkoani Katavi wanalalamika kucheleweshwa kwa pembejeo za kilimo wakati wa msimu wa kilimo na malipo ya fedha za wakulima baada ya mauzo.
Habarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA