Posts

Showing posts from February 1, 2018

SERIKALI YAOMBWA KUWAANGALIA UPYA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR

Image
Mkurugenzi  Umoja wa watu wenye ulemavu Zanzibar Asia Abuu Salami  ameiomba serikali  na Taasisi mbalimbali za maendeleo nchini,kuwapa kipaumbele zaidi watu wenye ulemavu na wasiojiweza pindi zinapotokea   fursa za kimaendeleo kwa wananchi. Amesema  ni vyema Watu wenye ulemavu  kupewa haki sawa za kimaendeleo na watu wengine wasokuwa na ulemavu ili kila mmoja wao ajihisi huru kama wengine kwani nao wakiwezeshwa wanaweza. Aidha Mkurugenzi  Asia  amebainisha kuwa  bado watu wenye ulemavu  wanakabiliwa na changamoto  nyingi katika jamiii ikiwemo ukosefu wa vifaa wanavyotumia kwa shughuli zao za kila siku kama vigari vya kutembelea,Fimbo,Miwani na kadhalika. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Hassan Hatibu Hassan amewashauri watu wenye ulemavu  Mkoani humo kuanzisha Jumuiya  ya pamoja itakayowawezesha kurahisisha upatikanaji wa mahitaji yao. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MAHAKAMA KUU KENYA YABATILISHA UFUNGAJI WA VITUO VYA HABARI

Image
Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru kuwashwa kwa vituo vya habari vitatu binfasi na serikali na kuiagiza serikali kutoingilia utendaji kazi wa vituo hivyo hadi kesi hiyo itakaposikilizwa kikamilifu. Siku ya Jumanne matangazo ya vituo vya KTN,NTVna Citizen TV yalizimwa ghafla na serikali baada ya mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya kuzima mitambo yao kuepusha vituo hivyo kurusha moja kwa moja mkutano wa kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama Rais wa watu wa Kenya. Sherehe ya kuapishwa kwa Raila ilichukuliwa na wengi kama mzaha lakini serikali imeshikilia kuwa kitendo hicho kilikuwa kinakiuka sheria za nchi hiyo na kwamba ni kosa la uhaini hivyo ilijaribu kuhakikisha taarifa hiyo haitawafikia Wakenya wengi ambao wangelifuatilia tukio hilo kupitia matangazo ya luninga Okiya Omtata ambaye ni muwasilishaji mashtaka na mwanaharakati amesema anataka agizo la serikali litangazwe kuwa kinyume na katiba na vituo hivyo vifidiwe. Wakenya wengi wamekosa matangazo ya run

ORODHA YA MIKOA NA NAFASI ZAO KATIKA UFAULU WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2017

Image

RAIS ASEMA ATAJUA ATAKAVYOFANYA WATAKAOBORONGA MAHAKAMANI, AWABADILIKIA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI PIA WAZIRI WA SHERIA

Image
Rais wa Tanzania Dkt.John Magufuli alisema bado kuna tatizo kubwa katika ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) na AG (Mwanasheria Mkuu),na ndiyo maana muda mwingine inawapelekea kuwapa changamoto kubwa Majaji. Kwa upande mwingine,Rais Magufuli amewataka viongozi wengine wanaosimamia vyombo vya sheria kufuata mfano mzuri aliyouanzisha Profesa Ibrahimu Juma kwa kutowafumbia macho wahalifu wa aina yeyote ile. Rais ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hizo aliongozana viongozi wengine wa serikali. Wakti huo huo Rais  Dkt.Magufuli leo amewabadilikia Waziri wa Katiba na Sheria,Prof.Palamagamba Kabudi na Mwanasheria Mkuu wa serikali,George Masaju na kudai kuwa wanakwamisha haki kutendeka kwa watu kutokana na kutofanyia kazi mambo ya msingi. Amesema yeye ameumbwa kusema ukweli hivyo ataendelea kuusema hata kama kuna watu unawaumiza. Wakati huo huo Rais Magufuli kupitia kilele cha maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria amewapa pole Majaji kwa changamoto wanazokumba