MTANZANIA AHUKUMIWA KUNYONGWA UGANDA

Mahakama Kuu nchini Uganda imemuhukumu Mtanzania kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji.
Mtanzania huyo aliyetambulika kwa jina la Matule Chresporeto Coleheri mkazi wa Bukoba anadaiwa kumuua mfanyakazi mwenzake katika shamba moja lililoko eneo la Wakyuto wilayani Nakaseke.
Akisoma hukumu hiyo,Jaji Steven Mubiru amesema baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka,mahakama imejiridhisha kuwa Matule ndiye alitenda kosa hilo.
Amesema  mashahidi watatu walioshuhudia tukio hilo wameiridhisha mahakama kuwa Thomas Kamuhebwa aliuawa na mtuhumiwa huyo.
Mwili wa Kamuhebwa ulikutwa ukiwa umetupwa katika shimo moja na kufungwa katika begi hali iliyosababisha mwili kuokotwa  karibu na makazi ya mshtakiwa.
Hata hivyo,mbele ya mahakama hiyo Matule alijitetea kutohusika katika mauaji hayo na kudai tuhuma hizo zilitengenezwa na watu waliotaka kuiba magogo yake aliyoyaandaa kwa ajili ya kuzalisha mkaa.
Awali,ilielezwa mahakamani hao kuwa Matule ni mhamiaji kutoka Tanzania aliyekuwa akifanya kazi za vibarua na kwamba Februari 6 mwaka,2014 alimuua Kamuhebwa kwa sababu zisizojulikana na kufukia mwili wake katika shimo.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA