Posts

Showing posts from February 10, 2018

RAIS MAGUFULI AMPANDISHA CHEO NA KUMTEUA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amempandisha cheo na kumteua Bw.Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Taarifa ambayo imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imefafanua kuwa Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Bw.Mohamed Hassan Haji kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP)na kisha kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar. Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji amepandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar kuanzia leo Februari 10 ambapo kabla ya uteuzi huu Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji alikuwa Mhasibu Mkuu wa Polisi Zanzibar. Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Hamad Omar Makame ambaye amestaafu. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

TANZANIA YARIDHIA KUFUTA TOZO YA DOLA ZA KIMAREKANI

Image
Tanzania imeridhia kufuta tozo ya Dola za Kimarekani 40 inayotozwa kwa kila stika katika magari yanayosafirisha mizigo kwenda nje ya nchi. Hatua hii imefikiwa katika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara,Viwanda,Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao umeafnyika Jijini Arusha Akizungumza katika Mkutano huo,Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage amesema Tanzania imefikia hatua hii ikiwa ni moja ya jitihada za kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini na Jumuiya kwa ujumla. Tozo hii imekuwa ikitozwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa malori yanoyosafirisha mizigo kwenda sehemu mbalimbali nje ya mipaka ya nchi. Mkutano huu uliofanyika Februari 7 mpaka 9 mwaka huu pamoja na mambo mengine ulilenga kujadili na kutatua vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru ambavyo vimekuwepo kwa muda mrefu katika Jumuiya. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA MAAMUZI YA UN

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ameelezea kusikitishwa na uamuzi wa Umoja wa Mataifa kuanza kutekeleza sera ya kupunguza gharama kwenye misheni za kulinda amani. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati wakizungumza na mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa wanaziwakilisha nchi zao hapa nchini mkutano ambao umefanyika ikulu jijini Dar es salaam. Amesema hatua hiyo itadhohofisha jitihada za kutafuta amani kwenye maeneo yenye migogoro na kuhatarisha maisha ya walinda amani pamoja na raia wasio na hatia wanaoishi kwenye maeneo yenye migogoro. Wakati huo huo pamoja na mambo mengine Mhe.Rais Magufuli amesema pamoja na nia njema ya mpango wa majaribio wa kutafuta suluhu la kudumu ya tatizo la wakimbizi,Tanzania imeamua kujitoa kutokana na changamoto za kiusalama na ukosefu wa fedha za kugharamia mpango huo. Wakati huo Rais Magufuli amesema Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wakiwemo wa kimataifa wote wanaohitaji kuwekeza hap

KIM JONG-UN AMUALIKA RAIS WA KOREA KUSINI

Image
Kiongozi wa taifa la Korea Kaskazini Kim Jong un amemualika rais wa Korea Kusini Moon Jae-in kuzuru Pyongyang ambapo Utakuwa mkutano wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja kati ya viongozi hao wa Korea. Rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini Bw.Moon amesema Korea ni muhimu kuhakikisha mkutano huo unafanyika huku akiitaka Korea Ksakzini kurudi katika meza ya mazungumzo na Marekani. Mualiko huo ulioandikwa ulikabidhiwa kwa rais wa Korea Kusini na dadake rais Kim Jong un,Kim Yo Jong ambapo Katika mkutano wa kihistoria uliofanyika katika jumba la rais kabla ya kuanza kwa michezo hiyo ya msimu wa baridi. Bi.Kim na kiongozi wa kisherehe wa taifa la Korea Kaskazini Kim Yong-nam ndio viongozi wa ngazi za juu kutoka Kaskazini kuzuru kusini tangu vita vya Korea 1950. Rais Donald Trump na mwenzake wa Korea Kusini Kim Jae-in Wakati huohuo Rais wa Korea ya Kusini Moon Jae amekuwa ni mwenye shughuli nyingi za kupokea ujumbe wa ngazi ya juu katika ikulu yake ya mjini Seoul

MH.SUGU NA MASONGA WAACHIWA KWA DHAMANA HUKUMU YAO FEBRUARI 26,2018

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi-Mbeya imewaachia kwa dhamana washtakiwa Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi''SUGU'' na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga.

RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA NA MABALOZI NA WAKUU WA MASHIRIKA YA KIMATAIFA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Joseph Magufuli amewahakikishia mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa waliopo hapa nchini kuwa katika kipindi cha mwaka 2018 serikali ya awamu ya tano itaendeleza juhudi za kuendeleza mazingira ya uwekezaji ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa,kuboresha miundombinu ya barabara,reli na usafiri wa anga,kuongeza uzalishaji wa umeme na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia Mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa waliopo hapa nchini kuwa katika mwaka 2018 Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza juhudi za kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, kuboresha miundombinu ya barabara, reli na usafiri wa anga, kuongeza uzalishaji wa umeme na kukabiliana na vikwazo vya biashara. Mhe. Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 09 Februari, 2018 katika hafla ya mwaka mpya aliyowaandalia Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao