KIM JONG-UN AMUALIKA RAIS WA KOREA KUSINI


Kiongozi wa taifa la Korea Kaskazini Kim Jong un amemualika rais wa Korea Kusini Moon Jae-in kuzuru Pyongyang ambapo Utakuwa mkutano wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja kati ya viongozi hao wa Korea.
Rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini
Bw.Moon amesema Korea ni muhimu kuhakikisha mkutano huo unafanyika huku akiitaka Korea Ksakzini kurudi katika meza ya mazungumzo na Marekani.
Mualiko huo ulioandikwa ulikabidhiwa kwa rais wa Korea Kusini na dadake rais Kim Jong un,Kim Yo Jong ambapo Katika mkutano wa kihistoria uliofanyika katika jumba la rais kabla ya kuanza kwa michezo hiyo ya msimu wa baridi.
Bi.Kim na kiongozi wa kisherehe wa taifa la Korea Kaskazini Kim Yong-nam ndio viongozi wa ngazi za juu kutoka Kaskazini kuzuru kusini tangu vita vya Korea 1950.
Rais Donald Trump na mwenzake wa Korea Kusini Kim Jae-in
Wakati huohuo Rais wa Korea ya Kusini Moon Jae amekuwa ni mwenye shughuli nyingi za kupokea ujumbe wa ngazi ya juu katika ikulu yake ya mjini Seoul baada ya ufunguzi rasmi jana wa michezo ya Olympic ya msimu wa baridi nchini humo ambapo jana amesalimiana na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un.
Ulikuwa ni mara ya kwanza ujumbe kama huo wa maafisa wa ngazi za juu zaidi wa Korea Kaskazini kuwahi kuzuru Korea Kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea miaka 60 iliyopita ambapo hata hivyo hatua hiyo haijafurahiwa na Marekani.
Makamu rais wa Marekani,Mike Pence alisusia mwaliko wa chakula cha jioni ambacho alitakiwa kukaa meza moja na kiongozi wa serikali ya Korea Kaskazini Kim Yong-nam.
Taarifa kutoka chombo cha habari cha Yo hap kimesema Pence alionana kidogo na bw.Kim wakati wakijaribu kukwepana kuonana uso kwa uso.
Michezo hiyo inaendelea wakati ambapo kuna mvutano juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini ambao unapingwa vikali na majirani zake na vilevile Marekani.
Katika shughuli hiyo,Bw.Moon alisema anatarajia mashindano hayo ya michezo ya Olimpiki msimu wa baridi yataweza kukumbukwa kama siku nzuri ya kuanza kuwa na amani.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA