MH.SUGU NA MASONGA WAACHIWA KWA DHAMANA HUKUMU YAO FEBRUARI 26,2018


Mahakama ya Hakimu Mkazi-Mbeya imewaachia kwa dhamana washtakiwa Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi''SUGU'' na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga.

Mh.Mbilinyi  na Masonga ambao wameachiwa jana wamekuwa mahabusu kwa muda wa siku 24 baada ya kunyimwa dhamana na mahakama hiyo kutokana na hoja za upande wa  Jamhuri.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite amewaachia kwa dhamana wawili hao baada ya Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala kuiambia mahakama hiyo kwamba imeshafunga ushahidi wake ambapo mashahidi sita walitoa ushahidi wao.

Mawakili wa pande zote mbili walikubaliana kuwa Februari 19 watawasilisha majumuisho ya shauri hilo mahakamani hapo ambapo hakimu Mteite amekubaliana  na hoja hiyo ya mawakili na kusema hukumu ya kesi hiyo itatolewa Februari26 mwaka huu.

Mh.Mbilinyi  na Masonga wanakbiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA