Posts

Showing posts from March, 2018

JUMAMOSI KUU

Image
Jumamosi kuu  ni  siku  ya  Juma kuu  inayoadhimisha hasa  pumziko  la  mwili  wa  Yesu Kristo   kaburini  kabla ya  kufufuka  kwa  utukufu   usiku  wa kuamkia  Jumapili  ya  Pasaka . Tarehe  yake inabadilikabadilika kila  mwaka  na hata mwaka uleule ni tofauti katika  madhehebu  ya  Ukristo , hasa yanayofuata  mapokeo  ya  mashariki  na yale yanayofuata mapokeo ya  magharibi . Siku hiyo  Misa  na  sakramenti  mbalimbali haziadhimishwi kwa kuwa  wafuasi  wa  Yesu  wanatulia  kimya  wakitafakari matukio ya  Ijumaa kuu  na kujiandaa washangilie  ufufuko wake kuanzia  kesha  la Pasaka hadi  Jumapili  ya  Pentekoste  siku  50  baadaye. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

MKUU WA WILAYA AIBULIWA NA SHULE KUITA WAGANGA KUTOKA KONGO

Image
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mohamed Mtanda ametolea ufafanuzi suala la shule ya Msingi Kabwe kuita waganga wa kienyeji kutoka Kongo ili kutatua tatizo la kishirikina linaloikabili shule hiyo.` Mtanda amesema ni kweli alipokea simu kutoka kwa Mkuu wa shule hiyo kumuelezea matatizo yao hapo shuleni na lengo walilofikia serikali ya kijiji ili kutatua tatizo hilo ambalo limekuwa likijitokeza mara kwa mara. Licha ya hayo,mkuu wa wilaya hiyo amesema yeye kama kiongozi wa serikali ni kulichukua tatizo hilo kitaalam kwa kupeleka madaktari ambao watatafuta njia sahihi ya kutibu wanafunzi hao na sio kuruhusu mambo ya kishirikina ingawa hawezi kuwakataza wazee wa kijiji hicho kwani anaheshimu mila zao. Wanafunzi wa kike wa shule ya msingi Kabwe iliyopo Wilayani Nkasi mkoani Rukwa wanakabiliwa na tatizo la kiafya la kuanguka,kuzimia na kupiga kelele jambo ambalo wakazi wa eneo hilo wanahisi linatokana na ushirikina na kuamua kutafuta waganga wa kienyeji ili kutafuta ufumbuzi. Chanzo:ea

ASKOFU NYAISONGA ATAKA WAKRISTO WATENDE MEMA

Image
Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga Katika maadhimisho ya siku ya Ijumaa kuu kwa wakristo,Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda Mkoani Katavi   Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga amewataka waumini wa kikristo kuendelea kutenda kutenda mema kama walivyofanya katika kipindi cha mfungu wa Kwaresma. Askofu Nyaisonga ametoa wito huo leo katika adhimisho misa takatifu ya Ijumaa kuu katika ibada ambayo imefanyika katika Kanisa kuu la Bikira Maria Emakulata Jimbo la Mpanda. Kwa upande wao waumini wa kanisa hilo wamesema kipindi cha Kwaresma ni kipindi cha kutafakari wema ambao mungu ameuonesha kwao na hivyo kutakiwa kutenda hivyo hivyo kwa wenye uhitaji. Ijumaa Kuu ni siku maalumu ya mwaka ambayo wafuasi wengi wa Yesu Kristo wanaadhimisha kifo chake msalabani ambacho kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu siku ya Ijumaa ambapo inatanguliwa na Alhamisi Kuu. Sikukuu ya pasaka kwa mwaka 2018 inatarajiwa kuadhimishwa Aprili mosi mwaka huu. Ijumaa kuu kitaifa imeadhimishwa M

IJUMAA KUU

Image
Ijumaa Kuu  ni  siku  maalumu ya  mwaka  ambayo  wafuasi  wengi wa  Yesu Kristo  wanaadhimisha  kifo  chake  msalabani  ambacho kilitokea nje ya kuta za  mji  wa  Yerusalemu  siku ya  Ijumaa . Kadiri ya  Injili  ya  Mtume Yohane ,kesho yake ilikuwa  Sabato  na pia  Pasaka ,jambo lisilotokea kwa kawaida. Kwa sababu hiyo  wataalamu  mbalimbali wanakadiria ilikuwa tarehe  7 Aprili   30 . Ijumaa kuu ni sehemu ya  Juma Kuu  linaloanza kwa adhimisho la  Yesu  kuingia mji huo akishangiliwa kama  mfalme wa Wayahudi  (yaani  Masiya  au  Kristo ).Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa  wiki , yaani  Jumapili ya matawi . Ijumaa kuu ni pia sehemu ya  siku tatu kuu za Pasaka  zinazoadhimisha mateso na  kifo chake  ( Ijumaa ), kulala  kaburini  ( Jumamosi ), na hatimaye  kufufuka  kwa  utukufu  ( Jumapili ), kwa ufupi: Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka. Jana ilikuwa Alhamisi KUU Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

MKOANI KATAVI AMUUA MKEWE NA KUZIKA MWILI WAKE

Image
Jeshi   la   Polisi mkoani Katavi   linamshikilia mkazi   wa   Kijiji   cha   Songambele   Kata ya   Sibwesa   Tarafa ya   Karema Wilaya ya   Tanganyika   jina   lake   limehifadhiwa(45) kwa   tuhuma za kumuua mke   wake(31) kwa sababu ya wivu wa kimapenzi na   kisha mzika huku   mtoto wake mwenye   umri wa miaka tisa akishuhudia tukio. Kamanda wa   Jeshi la   Polisi wa   mkoa   wa   Katavi    Damas    Nyanda     alisema tukio   la kupatikana   kwa   mwili   wa   marehemu   huyo lilitokea juzi majira ya saa 6;00 mchana   katika Kijiji   hicho. Alisema   marehemu aliuawa   na   mumewe huyo siku ya   januari 15   kwa   kupigwa na   mumewe   kwa   kutumia silaha   zajadi ambazo ni fimbo na   mpini   wa    jembe baada ya   kumtuhumu kuwa   anamahusiano wa   kimapenzi na wanaume   wengine   Kijijini   hapo. Kamanda    Nyanda alisema wakati mtuhumiwa   huyo akitenda kosa hilo    ambalo   lilishuhudiwa   na   mtoto   wake wa kiume hadi    baba   yake   alivyomuuawa   mama   yake   na

WATOTO WA KANISA KATOLIKI WATOA MSAADA KWA WAGONJWA HOSPITALI YA MANISPAA YA MPANDA

Image
Katika kuadhimisha Alhamisi kuu kuelekea sikukuu ya pasaka,Watoto wa shirika la mtoto yesu kutoka jumuiya mtakatifu Filomena kigango cha Kawajense Majengo Mapya jimbo katoliki la Mpanda Mkoani Katavi,wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda. Wakizungumza kwa niaba ya watoto wenzao Sesilia John Enock na Samweli wamesema wameamua kutoa msaada kwa wagonjwa wenye uhitaji ikiwa ni kuadhimisha Alhamisi kuu katika kuelekea sikukuu ya pasaka. Jimbo Katoliki la Mpanda Katavi(PICHA NA.Issack Gerald) Kwa upande wake Katekista Joseph Paul Kansato ambaye pia ni mwalimu wa parokia ya kanisa kuu jimbo la Mpanda amesema watoto hao wametoa misaada mbalimbali ikiwemo sabuni, mafuta na sukari kama ishara ya upendo walionao kwa watu wenye shida mbalimbali. Kwa upande wao baadhi ya wagonjwa wakiwemo Mussa Paul na Magreth Peter Ndekeja wametoa shukrani zao kwa watoto hao waliotoa msaada huo huku wakiomba jamii kuiga mfano uliooneshwa na wato

IGP SIRRO AWAHAKIKISHIA USALAMA WATANZANIA WOTE KIPINDI CHA PASAKA

Image
Amesema Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro matukio  makubwa ya uhalifu wa kutumia Silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini. IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari ili kutoa salaamu za pasaka kwa watanzania ambapo amewashukuru Wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa Jeshi la Polisi  jambo ambalo limesaidia kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa hapa nchini.  Aidha amesema jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili  kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia. Katika hatua nyingine amesema jeshi la Polisi katika mikoa yote linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu hii inasherekewa kwa amani na utulivu na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka. Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia,fukwe,sehemu za starehe n

DKT.SHEIN AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Viongozi walioapishwa na Rais Dk.Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Fatma Gharib Bilal ambaye ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee, Wanawake na Watoto na Abdalla Hassan Mitawi ambaye ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid,Jaji Mkuu wa Zanzibar   Omar Othman Makungu,Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said pamoja na Mawaziri. Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih,Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,Mkuu wa   Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud,Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine

RIPOTI YA DAKTARI KUHUSU WALIOKUFA KWA SUMU YA UYOGA KATAVI HII HAPA

Image
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Dkt. Theopister Elisa amesema uchunguzi wa kitabibu unaonesha mwanamke Mariana Gerald Sanane(47) mkazi wa kijiji cha Sitalike Wilayani Mpanda aliyefariki duniani baada ya kula uyoga unaotajwa kuwa na sumu aliathiriwa katika ini. Dkt.Theopister Elisa ameeleza hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari kueleza walichokibanini kwa mwanamke huyo baada ya kufariki kwa kula uyoga ambao unadaiwa kuchumwa kutoka zizi la ng’ombe baada ya uyoga huo kumwagiwa dawa ya kupulizia ng’ombe. Aidha Dkt.Elisa amesema waathiriwa wa sumu hiyo walicheleweshwa kufikishwa katika vituo vya huduma za afya hali iliyosababisha mathara makubwa kujitokeza mwilini mpaka kusababisha mauti baada ya idi kuathirika. Machi 25 mwaka huu Frenki Mayaga na Erizabeth George wakazi kijiji cha Sitalike wakiwa wa familia moja,walifariki dunia baada ya kula uyoga huo wenye sumu na hivyo kufikisha idadi ya watu watatu waliofariki dunia wote wakitoka katik

HIACE YAUA MWALIMU WA SEKONDARI KATAVI

Image
Mwalimu wa shule ya sekondari ya St.Mary’s iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Hipoliti Julius Milambo amefariki dunia papo hapo baada ya kogongwa na gari aina ya hiace. (Hiyo picha haina mahusiano na habari hii) Kwa mjibu wa mashuhuda,ajali hiyo ilitokea jana majira ya jioni ambapo marehemu aligongwa katika eneo la Mpanda Hotel na gari lililokuwa likitoka kata ya Kakese ambapo aligongwa wakati akivuka barabara. Aidha wametaja gari ambalo lilimgonga mwalimu huyo kuwa ni Hiace Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Theopister Elisha akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake amesema hajapata ripoti ya kifo cha mwalimu huyo. Hata hivyo kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda alipotafutwa kuelezea tukio hilo amedai kuwa yupo msibani. Wakati huo huo waendeshaji wa vyombo vya moto wameshauri kuwekwa matuta katika barabara inayotoka Mpanda – Kigoma   ili kupunguza ajala za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea. Habari kamil

WANANCHI WALALAMIKIA UONEVU KATAVI

Wananchi wa kitongoji cha Itogolo katika kijiji cha Kampuni   kata ya misunkumilo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameilalamikia serikali kuwakamata,kuwatoza faini na kuwalazimisha kuvuna mazao yao kabla ya kukomaa. Wananchi hao wakiwemo Agnes John,Charles Pius na Peter Luamula wametoa malalamiko hayo katika mkutano wa hadhara wa kijiji cha Kampuni ambapo ulikuwa ukifanyika katika kitongoji hicho lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa wananachi kueleza kero zao. Wamesema wamekuwa wakikamatwa ovyo na mgambo kisha kupelekwa mahabusu na kulipishwa faini wakati hakuna elimu ya kutambua mita sitini kutoka chanzo cha maji ya mto Mpanda iliyotolewa. Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya watumia maji bonde la mto Mpanda Mahela Mahanda na Daudi Sumuni wamekanusha kuwaamrisha wananchi kuvuna mazao yao kabla ya kukomaa lakini wamekubali kuwakamata na kuwatoza faini kabla ya kutoa elimu kwa wananchi hao. Mwenyekiti wa kijiji cha Kampuni Bw.James Simoni amesema mpaka sasa watu wa

WAKURUGENZI WATATU WATUMBULIWA WAWILI WA KIGOMA

Image
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo   amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili kati ya watatu wa Halmashauri za Pangani na Kigoma baada ya kupata hati chafu katika matokeo ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2016/17. Ripoti hiyo iliyowasilishwa leo Machi 27, 2018 inaonyesha halmashauri 166   kupata hati safi,16 hati zenye shaka na halmashauri tatu kupata hati chafu. Umauzi huo unafanyika ikiwa ni dakika chache baada ya Rais John Magufuli kutoa agizo hilo. Halmashauri zilizopata hati chafu ni Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya Kigoma na Pangani. Waziri Jafo amesema baada ya kuwasimamisha,amemwagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuunda timu ya watalaamu kuchunguza hati hizo na kutoa matokeo ndani ya wiki tatu. Amesema wakurugenzi waliohusika katika hati chafu ni Daud Mlahagwa (Pangani),aliyekuwa Mkurugenzi wa Kigoma Ujiji, Judethadeus Mboya ambaye amestaafu kwa sasa na

MKUU WA SHULE AJINYONGA OFISINI KWAKE AKIMTAJA MKURUGENZI

Image
MKUU wa Shule ya Sekondari Kakonko wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Peter Rubonya amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba ofisini kwake mapema leo asubuhi. Akielezea tukio hilo,Mwalim wa zamu wa shule hiyo Isaac Japhet amesema yeye alifika shuleni hapo saa 12:30 asubuhi ili kuwafundisha wanafunzi wa kidato cha nne masomo ya ziada baada ya kufunga shule wiki iliyopita na baada ya kufika aligundua kuwa hana chaki ambapo mkuu huyo wa shule alimpatia chaki mlinzi ili awape wananfunzi. Amesema baada ya muda,Mratibu elimu kata pamoja na mmoja wa wazazi walifika ofisini hapo wakiwa na shida na mkuu wa shule na baada ya kuelezwa yupo ndani ofisini lakini baada ya kugonga mlango hawakuweza kujibiwa na ndipo wakaamua kufungua mlango na kukuta mwili wa marehemu ukining’inia dalini. Mwalim Isaac amesema Mwalimu aliyejinyonga alikuwa akifundisha masomo ya Kemia na Fizikia shuleni hapo hawakuwahi kusikia mgogoro wowote wa kifamilia au kijamii na mkewe ambaye ni mkufunzi katika Chuo Kiku

UYOGA WAUA MWINGINE KATAVI

Image
Mtu mwingine mkazi wa kijiji cha Sitalike wilayani Mpanda Mkoani Katavi amefariki dunia akiwa hospitali ya Manispaa ya Mpanda akipatiwa matibabu na hivyo kufikisha idadi ya watu watatu waliofariki kutokana na kula uyoga unaosadikiwa kuwa na sumu. Mwenyekiti wa kijiji cha Sitalike Bw.Christopher   Anjero amemtaja mwanamke aliyefariki leo kuwa ni Mariana Gerald Sanane ambaye ni Mama wa marehemu wawili waliofariki siku ya jana. Waliofariki jana kutokana na kula uyoga huo ni Frenki Mayaga   ambaye alifariki akipatiwa huduma ya kwanza katika kijiji cha Stalike huku   Erizabeth George ambaye alikimbizwa hospitali ya Manispaa ya Mpanda akiaga dunia baada ya kufikishwa katika mlango wa Daktari. Mganga wa zamu wa hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambaye alitakiwa kueleza zaidi kuhusu suala hilo amekana kuzungumza kwa madai ya kutokuwa msemaji kwa sasa. Kisa hicho   ambacho kimeacha simanzi kwa jamii kutokana na vifo vya watu watatu wa familia moja kinatajwa kuwa ni kuwa cha kwanza kati

RAIS MAGUFULI APOKEA NA KUZINDUA MAGARI 181 YA MSD,MIKOA MIPYA YATAJWA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli amesema serikali inaendelea kupanga   mikakati yake kuhakikisha inakarabati na kujenga vituo na Hospitali zinazotoa huduma za afya nchini ikiwemo mikoa mipya ya Katavi,Songwe,Geita,Simiyu na Njombe. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo katika hafla fupi ya ugawaji wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini,uzinduzi ambao umefanyika eneo la Keko jijini Dar es Salaam. Aidha Rais Magufuli mbali na kuwashukuru Global Fund kwa msaada wa magari 181 yasiyokuwa na   masharti amesema yatarahisisha huduma mbalimbali katika maeneo ya Tanzania katika sekta ya afya. Awali Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa Nchini MSD Laurean Rugambwa Bwanakunu,amesema magari ya bohari ya dawa MSD sasa yatakuwa 213 kutoka magari 32 yaliyokuwepo ambapo magari hayo ya Land Cruiser 104,Malori 77 ambayo kwa ujumla yamegarimu shilingi Bilioni 20.75. Kwa upande wake Leindan Moris mwakailishi wa Global Fund

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

Image
Jokate Mwegelo Jokate Mwegelo Amezaliwa Jokate Urban Mwegelo 20 Machi   1987   (umri 31) 20 Machi   1987   (umri 31) Utaifa MTanzania Mhitimu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ( Shahada ya Sayansi ya Siasa ) Kazi yake Mwigizaji, mjasiriamali, mtangazaji, mwimbaji Miaka ya kazi 2006-hadi sasa Jokate Mwegelo  ni  mwigizaji  wa  filamu  na mjasiriamali kutoka nchini  Tanzania . Jokate vilevile ni mtangazaji na mwimbaji. Huyu ni  Afisa Mtendaji Mkuu  wa kampuni ya  Kidoti Company .Mwaka wa 2011,alishinda tuzo ya  Zanzibar International Film Festival  akiwa kama mwigizaji bora filamu wa kike.Mwaka wa 2017,Mwegelo aliingizwa katika jarida la Forbes katika  Forbes 30 Under 30  kutoka Afrika. MAISHA YA AWALI NA ELIMU. Mwegelo alizaliwa mnamo tarehe 20 Machi,1987 huko mjini  Washington D.C ambapo wakati huo wazazi wake walikuwa wanafanya kazi.Alikulia jijini  Dar es Salaam, Tanzania .Alianza elimu y