RAIS MAGUFULI APOKEA NA KUZINDUA MAGARI 181 YA MSD,MIKOA MIPYA YATAJWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli amesema serikali inaendelea kupanga  mikakati yake kuhakikisha inakarabati na kujenga vituo na Hospitali zinazotoa huduma za afya nchini ikiwemo mikoa mipya ya Katavi,Songwe,Geita,Simiyu na Njombe.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo katika hafla fupi ya ugawaji wa magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini,uzinduzi ambao umefanyika eneo la Keko jijini Dar es Salaam.
Aidha Rais Magufuli mbali na kuwashukuru Global Fund kwa msaada wa magari 181 yasiyokuwa na  masharti amesema yatarahisisha huduma mbalimbali katika maeneo ya Tanzania katika sekta ya afya.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa Nchini MSD Laurean Rugambwa Bwanakunu,amesema magari ya bohari ya dawa MSD sasa yatakuwa 213 kutoka magari 32 yaliyokuwepo ambapo magari hayo ya Land Cruiser 104,Malori 77 ambayo kwa ujumla yamegarimu shilingi Bilioni 20.75.
Kwa upande wake Leindan Moris mwakailishi wa Global Fund amesema wametoa msaada huo ili kuwezesha bohari ya dawa MSD itoe huduma za jamii mara kwa mara katika vituo mbalimbali nchini.
Kwa mjibu wa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu kwa sasa Tanzania ina vituo vinavyotoa huduma za afya vipatavyo 7284.
Habari zaidi ni WWW.P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM




Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA