Posts

Showing posts from August 4, 2015

UKAWA WAMPITISHA RASMI LOWASSA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA

Image
  Edward Lowassa Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa NA MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM Chama cha demokrasia na maendeleo chadema   leo kimemuidhinisha Edward lowasa kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika   mwezi Oktoba mwaka huu.  Wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema uliofanyika   leo Jijini   Dar Es salaam wamepiga kura ya   kuridhia kiongozi huyo aliyejiunga na upinzani akitokea chama tawala CCM kuwa mgombea   Kiti hicho cha   urais   Kupitia chama hicho.  Mwanasiasa huyo Mkongwe hapa Nchini amekuwa   akiyagawa   maoni ya Watanzania tangu akihame chama cha Mapinduzi na Kuhamia chama cha   chadema   tang u vikao vya uteuzi vya ccm   kumpitisha mgombea wa urais kulikata jina lake. Hata hivyo katibu mkuu wa chadema Wilbroad Slaa hakuhudhuria mkutano huo mkuu Kutokana na kuwepo kwa taarifa kuwa hakufurahishwa   na uamuzi wa chadema kumpokea Lowasa. SOMA HAPA KUMFAHAMU LOWASSA

VIONGOZI WA UMMA TANZANIA WATAKIWA KUWA WAZALENDO KUPITIA WANAOWAONGOZA

  Na.Issack Gerald-KATAVI Viongozi wa umma hapa nchini wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Uzalendokatika kutekeleza mahitaji ya wanaowaongozana siyo kwa maslahi binafsi.

WENYE SIFA YA KUPIGA KURA KATAVI WATAKIWA KUHAKIKI MAJINA YAO KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA

Image
Nembo ya tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania Na.Tume ya taifa ya Uchaguzi-KATAVI WANANCHI   Mkoani Katavi wametakiwa Kufika katika Vituo vyao walivyojiandikishia   Katika daftari la Mpiga Kura ili kuhakiki taarifa zao   Katika daftari la hilo. Kwa Mjibu wa Tangazo lililotolewa na Tume ya taifa ya Uchaguzi NEC Zoezi hilo limeanza Augost Mosi mwaka huu ili kutoa fursa kwa wananchi waliojiandiksha Kuhakiki taarifa zao zilizokosewa kabla ya Muda wa Kupiga Kura. Jaji mstaafu Damian Lubuva mwenyekiti wa tume ya taifa ya Uchaguzio Tanzania Pamoja na Mkoa wa Katavi Mikoa mingine inayotakiwa kuanza zoezi hilo ni Rukwa,Njombe,Iringa,Mtwara,Lindi,Dodoma,Singida,Tabora na Kigoma.