Posts

Showing posts from January 3, 2018

MATUMIZI YA TOCHI BARABARANI MKOANI KATAVI ZATAJWA KUPUNGUZA AJALI KWA MWAKA 2017

Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoani Katavi limesema kuwepo kwa tochi za kudhibiti mwendokasi kumesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali za barabarani. Hatua hiyo imebainishwa na Askari wa kitengo cha Usalama Barabarani John Shindika wakati hali ya usalama katika kipindi cha mwaka 2017. Aidha Shindika amewataka watumiaji wa barabara kuwa makini wawapo barabarani ili kujiepusha na ajali zisizo za lazima. Katika hatua nyingine Shindika amesema suala la kuzuia ajali ni wajibu wa kila mtu hivyo kila mmoja yampasa kuzuia ajali kwa namna yoyote Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

JAMII WILAYANI MPANDA IMETAKIWA KUWAJALI WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU

Na.Issack Gerald Jamii mkoani katavi imetakiwa kuwajali watu wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali Wito huo umetolewa na Afisa ustawi wa jamii wa Manispaa ya Mpanda Bi.Agness Bulaganya ambapo amesema idara ya ustawi wa jamii inaendelea kutoa elimu shirikishi ili kuhakikisha jamii inapata uelewa wa kuishi na watu walio katika makundi hayo. Katika hatua nyingine Bi.Buraganya amesma endapo jamii inakuwa na mwamko wa kuwatambua watu walio kwenye makundi hayo,serikali mkoani Katavi iko tayari kuyaunganisha na fursa mbalimbali zitakazowawezesha kuijtegemea Amesema kwa mwaka wa 2018 idara ya ustawi wa jamii mkoani Katavi imejipanga kushughulikia masuala mbalimbali ikiwemo kupunguza ongezeko la mimba za utotoni. Kauli ya serikali kuhusu watu wenye mahitaji maalumu inakuja ikiwa ni siku moja baada ya shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu mkoani Katavi kusema kuwa serikali ya awamu ya tano haiwajali katika mahitaji yao kam

SUMATRA MKOANI KATAVI YAPONGEZWA KWA KUDHIBITI UPANDISHWAJI NAULI KIHOLELA MSIKUMU WA SIKUKUU

Image
Baadhi ya abiria mkoani Katavi wameipongeza mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na Nchi kavu (Sumatra) kwa kusimamia bei za nauli katika msimu wa sikukuu . Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema katika kipindi cha sikukuu mwaka huu bei za nauli hazikupanda ikilinganishwa na miaka iliyopita Aidha wamesema kupanda kwa nauli kunaleta usumbufu kwa abiria ambapo wameiomba Sumatra kuendelea kusimamia swala la bei za nauli mkoani  Katavi. Tatizo la upandishaji wa nauli kiholela limeripotiwa kutokea kwa mabasi yaliyokuwa yanafanya safari zake kutoka Arusha kwenda mikoa mingine katika msimu wa sikukuu hali hiyo ilisababishwa Sumatra kuingilia kati na abiria kurudishiwa fedha zao huku mamlaka hiyo ikisema hatua zaidi za kisheria kwa wote waliohusika na upandishaji nauli. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

SERIKALI MKOANI KIGOMA IMETATUA TATIZO LA UHABA WA ARDHI

Image
Jumla ya Hekta Elfu 10   sawa na hekari 26200 zimepunguzwa kutoka katika hifadhi ya Makere kusini wilayani Kasulu na Kugawiwa kwa wananchi wa vijiji   vya Mvinza na Kagerankanda. Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magafuli alilolitoa mwezi july mwaka jana wakati wa ziara yake Mkoani Kigoma lengo likiwa ni kwaongezea wananchi ardhi kwa ajili ya shughuli zakilimo. Akimwakilisha Rais,kaimu mkuu wa wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Kanal Malko Gaguti amesema,mara baada ya kufanya tathimini katika hifadhi hiyo imeonekana zaidi ya hekta 72 elfu za msitu wa Makere kusini kati ya hizo hekta elfu 18 zimeharibiwa vibaya kutokana na uvamizi wa shughuli za kilimo. Wahamiaji wanoingia nchini kinyume na sheria imeonekana kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa misitu lakini pia kufanywa kwa vitendo vya uharifu ambapo Gaguti ambapoa ametoa rai kwa wakazi wa vijiji Mvinza na Kagerankanda kutumia vizuri ardhi hiyo Wakitoa shukrani kwa serikali

ABUBAKAR SHEKAU AIBUKA TENA NA UJUMBE NCHINI NIGERIA

Image
Kiongozi wa kikundi cha wapiganaji wa Boko Haram Abubakar Shekau,ameonekana kwenye video mpya karibu saa ishirini na nne baada ya Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kwa mara nyingine kutamka hadharani kuwa kikundi hicho kimesambaratishwa. Image caption Kiongozi wa kikundi cha wapiganaji wa Boko Haram Abubakar Shekau Huu ni mkanda wa video wa kwanza kutolewa na Shekau baada ya kimya cha miezi kadhaa iliyopita huku akiwa ni mongoni mwa viongozi wanaosakwa kwa baada ya kupewa sifa ya kuwa miongoni mwa magaidi wanaosakwa na Marekani pamoja na mamlaka ya Nigeria. Abubakar Shekau anaonekana kwenye mkanda huo wa video akiwa ameketi peke yake akiwa amevalia kanzu,kofia yenye rangi inayofanana na bunduki aina ya AK-47 ambayo anaonekana kuwa na mahaba nayo Lakini anaonekana kushindwa kuzungumza kwa sauti yenye mamlaka ikilinganishwa na matamko yake ya awali . Akisoma kutoka katika karatasi kwa lugha ya kiarabu na ki Hausa,Shekau,anakiri kundi lake kuhusika katika matukio ya hivi karibu

WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI WAMEENDELEA KULIA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

Image
Na.Issack Gerald Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani Katavi Bw.Issack Mlela amesema Mkoa wa Katavi kushindwa kuwezesha maadhimisho ya watu wenye ulemavu mkoani Katavi ili yafanyike kunawaathiri kwa kuwa kero zao hazisikilizwi. Bw.Mlela amesema maadhimisho hayo hayakufanyika kwa miaka miwili mfulilizo mwaka 2016 na 2017 akisema baadhi yao kuwezshwa ili kushiriki yanakofanyika kitaifa ilishindikana na hivyo matatizo yao kuendelea kuwaandama bila kupatiwa ufumbuzi. Aidha Mlela ameiomba serikali kuwashirikisha watu wenye walemavu wanapopanga  bajeti ili kusaidia maadhimisho hayo kufanyika kwa siku maalumu kama inavyokuwa imepangwa kwa ajili ya kuwasilisha kero zao. Kwa mwaka 2017 serikali ilisema ilishindwa kuwezesha maadhimisho kufanyika Desemba 3 kam yanavyofanyika kila mwaka kimataifa kutokana na ukosefu wa fedha huku hata tarehe nyingine ya Desemba 19 iliyokuwa imepangwa kuadhimishwa siku ya watu wenye ulemavu duniani ikiahirishwa pia kutokana na

ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOANI KATAVI NA MIKAKATI YA KUFIKIA WILAYA ZOTE ZA MKOA

Image
Jeshi la zimamoto mkoani katavi limesema limejipanga vyema kuboresha huduma za jeshi hilo kwa mwaka wa 2018 ili kuweza kuzifikia wilaya zote za Mkoa wa Katavi. Kamanda wa Zimamoto na uokoaji mkoani katavi Abdallah Maundu amesema kwa jeshi la zimamoto nchini lilianzishwa miaka 10 iliyopita hivyo bado linaendelea kujitanua ili kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali Katika hatua nyingine kamanda Maundu amesema jeshi la zimamoto mkoani katavi litaendelea kutoa elimu kwa wananchi na kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ili kuweza kuwaepusha wananchi na majanga ya moto Aidha kamanda Maundu amesema katika sikukuu za Christmas na mwaka mpya hakukuwa na matukio ya kutishia uhai na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga na majanga mbalimbali katika sehemu wanakoishi Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED