ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOANI KATAVI NA MIKAKATI YA KUFIKIA WILAYA ZOTE ZA MKOA

Jeshi la zimamoto mkoani katavi limesema limejipanga vyema kuboresha huduma za jeshi hilo kwa mwaka wa 2018 ili kuweza kuzifikia wilaya zote za Mkoa wa Katavi.
Kamanda wa Zimamoto na uokoaji mkoani katavi Abdallah Maundu amesema kwa jeshi la zimamoto nchini lilianzishwa miaka 10 iliyopita hivyo bado linaendelea kujitanua ili kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali
Katika hatua nyingine kamanda Maundu amesema jeshi la zimamoto mkoani katavi litaendelea kutoa elimu kwa wananchi na kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali ili kuweza kuwaepusha wananchi na majanga ya moto
Aidha kamanda Maundu amesema katika sikukuu za Christmas na mwaka mpya hakukuwa na matukio ya kutishia uhai na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga na majanga mbalimbali katika sehemu wanakoishi

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA