SUMATRA MKOANI KATAVI YAPONGEZWA KWA KUDHIBITI UPANDISHWAJI NAULI KIHOLELA MSIKUMU WA SIKUKUU

Baadhi ya abiria mkoani Katavi wameipongeza mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na Nchi kavu (Sumatra) kwa kusimamia bei za nauli katika msimu wa sikukuu .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema katika kipindi cha sikukuu mwaka huu bei za nauli hazikupanda ikilinganishwa na miaka iliyopita
Aidha wamesema kupanda kwa nauli kunaleta usumbufu kwa abiria ambapo wameiomba Sumatra kuendelea kusimamia swala la bei za nauli mkoani  Katavi.
Tatizo la upandishaji wa nauli kiholela limeripotiwa kutokea kwa mabasi yaliyokuwa yanafanya safari zake kutoka Arusha kwenda mikoa mingine katika msimu wa sikukuu hali hiyo ilisababishwa Sumatra kuingilia kati na abiria kurudishiwa fedha zao huku mamlaka hiyo ikisema hatua zaidi za kisheria kwa wote waliohusika na upandishaji nauli.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA