HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA


Lazaro Nyalandu alizaliwa Agosti 18, 1970 mkoani Singida, hivyo atafikisha miaka 45 Agosti mwaka huu. Kwa sasa yeye ni Waziri wa Maliasili na Utalii.
Historia yake Lazaro Nyalandu alizaliwa Agosti 18, 1970 mkoani Singida.
Nyalandu alipata elimu ya msingi katika shule za Pohama na Mrumba zilizoko kijijini kwao huko mkoani Singida na kuhitimu mwaka 1987.
Aliendelea na masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Kibaha mkoani Pwani (1988 –1991) na alifaulu vizuri na kujiunga na Shule ya Sekondari Ilboru ambako alisoma kidato cha tano na sita.
Wakati akiwa mwanafunzi wa sekondari,Nyalandu alikuwa kiongozi wa juu wa Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania(Ukwata) 1991–1993 na baadaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania walioteuliwa kuzuru jiji la Rio De Janeiro,Brazil na kushuhudia mkutano wa Mazingira mwaka 1993.
Nyalandu alipata elimu yake ya Chuo Kikuu nchini Marekani ambako alihitimu Shahada ya kwanza ya Sanaa katika Usimamizi wa Biashara (BBA) mwaka 1997 katika Chuo Kikuu cha Wartburg.
Kabla ya hapo alikuwa amepata Shahada ya Biashara ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Wardorf nchini humo. Kiongozi huyu, ana Shahada ya Uzamili aliyoipata kwa njia ya utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Buckingham, Uingereza akifuzu katika masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diplomasia.
Baada ya kuhitimu masomo yake ughaibuni,Nyalandu alianza kazi huko huko Marekani katika Benki ya North West,akifanya kazi katika kitengo cha operesheni za kibenki kati ya mwaka 1998–1999.
Aliporejea nchini Tanzania alifanikiwa kuwa sehemu ya washauri wa mke wa aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa, katika uendeshaji wa taasisi ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).
Ushauri wa timu yake ulisaidia taasisi hiyo kupata misaada mingi kutoka nchi za Ulaya,Marekani,China na nyinginezo.
Pia,alikuwa anamsaidia mama huyo katika uandishi wa hotuba zake pale alipokuwa na majukumu makubwa ya kitaifa na kimataifa.
Nyalandu amemwoa mrembo wa Tanzania mwaka 2004 ‘Miss Tanzania’,Faraja Kotta na wana watoto wawili,Sarah na Christopher.
Mbio za ubunge
Tangu alipokuwa kijana mdogo,Nyalandu alionyesha kila dalili kuwa na nyota ya uongozi.Watu wanaomfahamu hawakushangaa walipomwona mwaka 2000 anaingia kwenye mpambano ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akilisaka jimbo la Singida Kaskazini.
Kutokana na udhaifu wa upinzani uliokuwepo wakati huo alijua atakuwa na kazi kubwa ndani ya chama chake tu, hivyo,alipopitishwa na CCM akapambana majukwaani na wapinzani na kuwa mbunge.
Mwaka 2005,Nyalandu alipitishwa tena na chama chake kuwania ubunge Singida Kaskazini,akakutana tena na upinzani dhaifu kutoka kwa Kimia Omari Rashid wa Chadema,akajivunia asilimia 93.5 ya kura zote na kuwa mbunge hadi mwaka 2010.
Baada ya kupata uzoefu wa ubunge,kwa miaka kumi, Nyalandu alirudi tena kutetea mara ya tatu;CCM ikampa nafasi mwaka 2010 na wananchi wakamchagua kwa ushindi wa asilimia 87.7 akimshinda kwa mara nyingine mgombea yuleyule wa Chadema wa mwaka 2005.
Ushindi wa mara hii ulikuja na bahati kubwa kwa Nyalandu.Bahati ya kwanza ilikuwa kukwea ngazi zaidi. Rais Jakaya Kikwete alimteua Nyalandu kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Novemba 2010 na alidumu hapo hadi Mei 2011 alipohamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii,nafasi aliyokaa kwa takriban miaka mitatu.
Bahati ya pili,Januari 2014,nyota yake ilipaa zaidi akapewa wadhifa mkubwa;mara hii akiteuliwa kuwa waziri kamili wa Maliasili na Utalii,sekta ambayo ina changamoto kubwa sana hapa nchini.

Mbio za urais
Nyalandu aliweka wazi nia yake ya kuwania urais Desemba 28,2014 na alitangaza nia hiyo ya kugombea urais katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Ilongero,katika jimbo analoliongoza,Singida Kaskazini, wakati akihutubia mamia ya wananchi.
Katika mkutano huo alisisitiza kuwa“sasa ni zamu ya vijana kuongoza nchi”huku akiwaambia wananchi kuwa safari yake ya ubunge kwa miaka 15 inaanzisha safari nyingine bila kuwaeleza ikiwa bado ana nia na ubunge au la.
Aliambatana na mkewe,watoto wake pamoja na wazazi wake.
Kabla ya kutangaza nia ya urais,Nyalandu aliwahi kusikika akisema kuwa “…siwezi kutangaza kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao bila kutumwa na watu” lakini kabla watu wenyewe hawajamtuma aliibuka na kuwaita yeye mwenyewe mkutanoni na kuweka nia yake.
Nguvu yake Nyalandu ni msomi mwenye jitihada kubwa. Si mwanasiasa mzembe au aliyekimbia umande; aliusaka kokote kule na leo hii anaweza kuingia kwenye mizani ya kupimwa kama mtu anayeweza kuongoza nchi au la. Nyalandu ana shahada tatu za chuo kikuu.
Tukumbuke kuwa amekuwa mtu wa karibu na mama Anna Mkapa kwa kipindi kirefu na mwanya huo aliutumia pia kuwa na mawasiliano na Rais Mkapa na hata alipokuwa mbunge akazidi kujijenga.
Baadhi ya makada muhimu ndani ya CCM wanamtaja vizuri na hii ni nafuu kubwa kwa mwanasiasa anayesaka kuingia Ikulu.
Pia,ana uzoefu wa kukaa bungeni kwa miaka 15.Huu ni uzoefu wa kipekee kabisa.Alipoingia bungeni,kwa mara ya kwanza,alikuwa kijana wa miaka 30 leo ana miaka 47. Utumishi wa chombo kikubwa kama Bunge kwa miaka 17 ni turufu muhimu sana kwake na inamwongezea sifa muhimu za kumbeba katika kinyang’anyiro.
Udhaifu wake
Pamoja na kutangaza nia ya kuwania urais,Nyalandu bado hajatangazika sana

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM