WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI WARIDHISHWA NA HATUA ZA SERIKALI KATIKA KUWAKWAMUA NA UMASKINI

Na.Issack Gerald-Katavi
WATU wenye ulemavu Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesema wameridhika na hatua zinazochukuliwa na Manispaa ya Mpanda katika kushughulikia mahitaji yao ikiwemo suala la mikopo.
Hayo yamebainishwa leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika shule ya msingi Azimio ukihusisha watu wenye ulemavu na wataalamu wa idara ya maendeleo ya mjamii Manispaa ya Mpanda kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kupata mikopo na uundaji vikundi vya kijasiliamali.
Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Mpanda Linus Kalindo pamoja na mambo mengine amewataka watu wenye ulemavu kutoona ulemavu ni mwisho wa maisha na badala yake waendelee kufuata nmna wanayoelekezwa ili wapatiwe mikopo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya watu wenye Ulemavu SHIVYAWATA Mkoani Katavi Issack Mlela amesema watazingatia yote wanayoshauriwa na wataalamu ikiwemo kuunda vikundi,kusajili vikundi na hatimaye kupatiwa mikopo.
Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwezi huu wa Oktoba kwa idara ya maendeleo ya jamii kukutana na makundi haya ya watu wenye ulemavu ili kusikiliza mahitaji yao na kuwaelekeza namna wanavyoweza kufanya ili kupata mikopo ya kujikwamua kiuchumi.
 Sheria namba 9 ya mwaka 2010 ilipitishwa na bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2010 kwa ajili ya kusimamia haki za watu wenye ulemavu hapa nchini katika masuala ya afya,elimu na haki nyingine za kibinadamu

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA