Posts

Showing posts from April 8, 2018

MAOFISA WA JESHI LA POLISI 458 WATIMULIWA KAZI

Image
Jumla ya maofisa wa Jeshi la Polisi wapatao 458 wamefukuzwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu kuanzia mwaka 2015 hadi Machi mwaka huu. Kauli hiyo imetolewa jana Aprili 7 na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro alipokuwa akizungumza mbele ya Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za Polisi na ufunguzi wa kituo cha Polisi cha Utalii na Kidiplomasia jijini Arusha. Sirro alisema kazi ya Jeshi la Polisi ni kurekebisha mienendo ya wananchi, hivyo kabla hawajawaelimisha wananchi wanapaswa kuwa na mienendo mizuri wao kwanza. Alifafanua kwa kulitambua hilo ndiyo maana askari waliokwenda kinyume na azma hiyo walichukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, ambapo kwa mwaka 2015, 198 walifukuzwa kazi. Alisema kwa mwaka 2016 walifukuzwa askari 165, 2017 (81) na kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu wamefukuzwa askari 14. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

POLISI RUKWA WAANZISHA OPARESHENI KUSAKA MASHAMBA YA BANGI.

Image
Jeshi la Polisi katika wilaya ya Kipolisi ya Raela Mkoani Rukwa limeanzishaa Oparesheni ya Kuyasaka mashamba yanayolima zao haramu ya bangi katika safu ya milima ya Lyamba Lyamfipa kwenye bonde la ziwa Rukwa. Mkuu wa Polisi katika wilaya hiyo ya kipolisi ya Raela Mrakibu mwandamizi wa polisi Aloyce Nyantola akizungumza leo wakati akishuhudia vijana kutoka kata ya Kapenta wilayani Sumbawanga wakivuna shamba la bangi lenye ukubwa wa heka 2 amesema walipata taarifa za kilimo hicho kutoka kwa raia wema na ndipo walipoanza kuzifanyia kazi. Katika Oparesheni hizo Nyantola ametoa wito kwa wananchi kuwa wema kuendelea kutoa taarifa huku akiwtaka pia kuzingatia sheria za nchi   na kuachana na kilimo cha mazao haramu. Kwa upande wake mkuu wa upelelezi wa wilaya hiyo ya kipolisi ya Raela mrakibu msaidizi Beda Msola amesema wananchi hao wamekuwa wakiendesha kilimo cha madawa ya kulevya ikiwemo bangi katika milima ya safu ya milima ya lyamba lyamfipa kwa kigezo kuwa maeneo ya msituni haya

RAIS MAGUFULI ASISITIZA SERIKALI KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA DINI KULETA MAENDELEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini katika masuala mbalimbali ya maendeleo hapa nchini. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo katika Ibada ya kumsimika Mhashamu Askofu Isaac Amani kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa la MtakatifuTeresia wa Mtoto Yesu Jijini Arusha. Mhashamu Askofu Isaac Amani aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi aliteuliwa na Baba Mtakatifu Francis tarehe 27 Desemba,2017 kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo na amesimikwa na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Mhashamu Josephat Louis Lebulu na Balozi wa Baba Mtakatifu hapa nchini Askofu Mkuu Marek Solczynski. Hatua ya rais Rais Magufuli kuhudhuria ibada hii ya kanisa katoliki imechukuliwa kama ishara bora ya kurejesha uhusiano mwema na baadhi ya makanisa makuu ya kikristo likiwemo kanisa katoliki ambao wamekua wakiikosoa vikali serikali yake.