MGANGA MKUU JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA
MHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemuhukumu mganga mkuu wa Zahanati ya Kasekese Wilaya ya Tanganyika Martin Mwashamba (27)kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la mbaka na kumpa mimba wanafunzi wa dasasa la sita wa shule ya Msingi Kasekese mwenye umri wa miaka 15 jina lake limehifadhiwa. Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya hiyo Odira Amwol baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka. Awali katika kesi hiyo mwendesha mashtaka Mwanasheria wa Serikali Mkoani Katavi Gregoli Mhagwa alidai Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai 2 mwaka jana Kijijini hapo. Alieleza Mahakamani hapo siku hiyo ya tukio mshitakiwa alimbaka mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita wa shule ya Msingi Kasekese mwenye umri wa miaka 15 huku akijua kufanya hivyo ni kosa. Upande