MGANGA MKUU JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA

MHAKAMA ya  Wilaya ya  Mpanda  Mkoani  Katavi   imemuhukumu mganga mkuu wa  Zahanati ya  Kasekese  Wilaya ya  Tanganyika  Martin  Mwashamba  (27)kifungo cha  miaka  30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la mbaka na kumpa  mimba  wanafunzi wa  dasasa la  sita  wa  shule ya  Msingi  Kasekese mwenye  umri wa miaka 15  jina  lake limehifadhiwa.

Hukumu  hiyo ilitolewa  jana   na   Hakimu  mkazi wa  Mahakama ya  Wilaya hiyo  Odira  Amwol   baada ya  Mahakama  kuridhika  na  ushahidi  uliotolewa  Mahakamani  hapo  na   upande wa  mashitaka.

Awali katika  kesi  hiyo  mwendesha  mashtaka   Mwanasheria wa   Serikali Mkoani Katavi  Gregoli  Mhagwa  alidai   Mahakamani  hapo  kuwa   mshitakiwa  alitenda  kosa  hilo  Julai  2  mwaka  jana   Kijijini  hapo.

Alieleza  Mahakamani  hapo siku  hiyo ya  tukio  mshitakiwa  alimbaka   mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa    darasa la  sita wa shule   ya   Msingi  Kasekese mwenye  umri wa  miaka   15 huku  akijua  kufanya  hivyo ni  kosa.

Upande wa  mashitaka   katika  kaesi  hiyo  uliongozwa  na  mwanasheria   Mhagwa ulikuwa na  mashahidi  watano na  miongoni  mwao  alikuwa ni  mwanafunzi   aliyetendewa kitendo hicho na  mshitakiwa   kwa  upande  wake wa utetezi   alikuwa na  mashahidi  watatu .

Hakimu  Amwol kabla ya  kusoma  hukumu  hiyo aliiambia   Mahakama  kuwa  kutokana  na  ushahidi  uliotolewa  Mahakamani  hapo na upande wa  mashitaka   Mahakama  pasipo  kuacha shaka  lolote   imemtia   mshitakiwa  hatiani kwa  mujibu wa kifungu  cha  sheria  130 kifungu  kidogo cha kwanza na chapili  na kifungu  cha  sheria   namba 131 kidogo cha kwanza  cha  kanuni ya  adhabu  sura ya 16  marejeo  ya  mwaka 2002.

Baada ya kutoa maelezo  hayo   Hakimu   alitaka  mshitakiwa  kama   anayosababu  yoyote ya  msingi ya   kuishawishi mahakama ili impunguzie   adhabu   basi   anapewa   nasafi hiyo kabla ya kusomewa  hukumu.

Mshitakiwa   Mwashamba Katika  utetezi  wake   aliiomba   Mahakama   impunguzie   adhabu   kwa  kile  alichodai   kuwa   yeye    anafamilia  inayomtegemea   na  pia   ana wadogo  zake  watatu   ambao   anawasomesha  yeye .

Hata  hivyo  utetezi  huo  ulipingwa  vikali na     mwendesha  mashitaka    mwanasheria wa  Serikali   Gregoli  Mhagwa  ambae   aliiomba  Mahakama  itoe  adhabu  kali  ili  iwefundisho kwa  watu  wengine  wenye  tabia   kama  hiyo .

Hakimu Amwol  baada ya  kusiliza  pande  hizo  mbili za   mashitaka  na  utetezi   aliiambia   Mahakama  kuwa   mahakama  imetowa   adhabu ya  kumuhukumu  mshitakiwa    Tabibu wa  Zahanati ya  Kasekese  Martin   Mwashamba  kutumikia  jela  kifungo cha  miaka  30 kwa  kosa  la  kumbaka    msichana  mwenye  umri wa miaka  16.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA