TRA KATAVI KUHAKIKI TIN NAMBA


Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoani katavi,imeanza kuhakiki namba za utambuzi(TIN NAMBA) kwa wafanya biashara waliosajiliwa katika biashara zao.
Meneja wa TRA mkoani Katavi Enos Mgimba amesema zoezi la uhakiki hili ambalo limeanzia leo Aprili 18,2018 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda baadaye litaendshwa katika maeneo mengine ya Mkoa.
Mgimba ametaja baadhi ya faida ya utambuzi wa TIN  NAMBA kwa TRA kuwa ni pamoja na mamlaka kuwa na taarifa sahihi za wafanyabiashara ili hali kukusanya mapato na kusaidia katika utatuzi wa changamoto mbalimbali za kibiashara.
Baadhi ya wafanyabiashara ambao wamefika katika zoezi hilo wamesema zoezi hilo lina faida kwao ikiwemo kutambulika katika biashara anayoifanya.
Halmashauri 5 za Mkoa wa Katavi zinazotakiwa kufanyiwa uhakiki ni Manispaa ya Mpanda na Nsimbo zinazopatikana Wilayani Mpanda,Mlele na Mpimbwe zinazopatikana Wilayani Mlele na ,Mpanda inayopatikana Wilayani Tanganyika.
Kwa mjibu wa Meneja Enos Mgimba,Jumla ya wafanyabiashara 4000 waliopo mkoani Katavi wanatarajiwa kuhakikiwa katika zoezi ambalo linatarajiwa kufikia tamati Aprili 27,2018.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA