Posts

Showing posts from February 15, 2018

MFAHAMU RAIS JACOB ZUMA AMBAYE AMEJIUZULU URAIS

Image
  Jacob Gedleyihlekisa Zuma   alizaliwa  Aprili 12, 1942 . Ni Rais wa  Afrika Kusini  tangu 2009.Alikuwa makamu wa rais chini ya  Thabo Mbeki  kati ya 1999 na 2005.Tangu Desemba 2007 ni mwenyekiti wa chama tawala cha  ANC . KIJANA NA MWANAHARAKATI WA ANC Alizaliwa kama mtoto wa wazazi maskini katika eneo la  Kwa Zulu-Natal .Akiwa na umri wa miaka 17 akajiunga na ANC akaingia katika upinzani mkali dhidi ya serikali ya  apartheid (ubaguzi wa rangi wa kisheria). Mwaka 1963 alikamatwa akafungwa jela miaka 10 huko  Robben Island  pamoja na  Nelson Mandela ambapo baada ya kuondoka gerezani akatoka Afrika Kusini akashiriki katika shughuli za nje za ANC huko  Msumbiji  na  Zambia na aliingia katika uongozi hadi kuwa mkuu wa ujasusi wa jeshi la ANC. KUPANDA NGAZI KATIKA AFRIKA KUSINI HURU Tangu ANC kuhalalishwa tena nchini Afrika Kusini mwaka 1990,Zuma alikuwa mwenyekiti wa chama cha  Natal  na baada ya uchaguzi wa 1994 akawa waziri katika serikali ya jimbo. Mwaka 1997

HATIMAYE RAIS ZUMA AJIUZULU

Image
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameamua kujiuzulu mara moja kufuatia kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa chama chake kinachotawala nchini humo cha African National Congress, ANC. Chama tawala nchini Africa kusini cha ANC,kimepokea tangazo la kujiuzulu kwa Rais Jacob Zuma katika nafasi yake ya Urais. Afisa mmoja mwandamizi wa chama hicho amesema hatua hiyo italeta utulivu wakati nchi inakabiliwa na changamoto mbalimbali. Ameongeza kwa kusema kuwa ANC haisherehekei hatua hiyo,kutokana na kuwa Zuma amekitumikia chama hicho kwa miaka 60. Awali kupitia televisheni Bw.Zuma alisema hakubaliani na mahitaji ya uongozi wa ANC kwamba anapaswa kujiuzulu, lakini amejiuzulu ili kuepusha ghasia ambazo zingechafua jina lake. Makamu wa Rais wa Africa kusini Cyril Ramaphosa atapigiwa kura na wabunge kama mkuu wa nchi na baadaye kula kiapo ndani ya siku chache zijazo. Zuma alikilalamikia chama cha ANC kwa kumtaka aondoke madarakani,ikiwa ni pamoja na kumtishia kumuondoa kupitia kura ya

BARAZA LA MADIWANI LACHARUKA UPIGAJI CHAPA MIFUGO CHINI YA KIWANGO

Image
BARAZA la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida limewajia juu wataalamu wake kwa kutotekeleza kwa weledi upigaji chapa mifugo na kuwatishia kuwa watalamika kwenda kurudia zoezi hilo kwa gharama zao iwapo alama zinazowekwa zitafutika baada ya muda mfupi.   Katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kilichofanyika Mjini Kiomboi, ajenda iliyochukua uzito mkubwa ni juu ya kufutika kwa alama zilizowekwa kwenye upigaji chapa mifugo na kuchelewa kwa malipo ya wananchi walioshiriki  kusaidia  utekelezaji wa zoezi hilo.  Afisa mifugo Wilaya ya Iramba Andrew Manyerere anasema kuwa ingawa zoezi hilo lilitekelezwa kwa kuzingatia sheria lakini kwa mifugo ambayo alama zake zimefutika watarudia  bila malipo. Hata hivyo uamuzi wa baraza la madiwani wa uliotolewa na Mwenyekiti wake Simion Tyosela ni kwa wataalamu kufanyakazi hiyo kwa weledi vinginevyo watarudia zoezi hilo kwa gharama zao. Zaidi ya shilingi milioni 16 zimetumika kuwalipa wanach

RAIS JACOB ZUMA ASEMA HAONI SABABU YOYOTE YA KUJIUZULU

Image
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma amesema hajafanya makosa na haoni sababu ya kujiuzulu. Bw.Zuma alizungumza baada ya chama tawala cha ANC kumtaka kujiuzulu vinginevyo atakabiliwa na kura isiokuwa na imani dhidi yake leo Alhamisi. Image caption Rais Jacob Zuma wa Afrika ya kusini amesema kuwa haoni sababu ya yeye kujiuzulu Rais huyo amekuwa chini ya shinikizo ya kujiuzulu huku kukiwa na madai mengi ya ufisadi lakini amesema ANC imeshindwa kuelezea ni kwa nini ametakiwa kujiuzulu. Bw.Zuma amesema yuko tayari kuondoka baada ya mwezi Juni lakini akapinga vile jambo hilo linavyoangaziwa kwa sasa na alisema atatoa taarifa nyengine baadaye siku ya Jumatano. Chama cha ANC kimesema kilisikiza matamshi ya Bw.Zuma lakini kitatoa uamuzi wa hatua yake baadaye kabla ya kuzungumza. Kiongozi wa chama hicho Jackson Mthembu alitangaza kuwa kura isiokuwa na imani dhidi ya rais itasikilizwa siku ya Alhamisi huku Cyril Ramaphosa aliyechaguliwa kuwa rais wa chama hicho mwezi Disemba akiap

MORGAN TSVANGIRAI AFARIKI DUNIA

Image
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika kusini. Kwa mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha MDC,Tsvangirai mwenye umri wa 65,na aliyewahi kushika nafasi ya Uwaziri mkuu nchini Zimbabwe ameripotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo. Marehemu Morgan Tsvangirai Makamu Rais wa chama chama cha MDC Elias Mudzuri amesema marehemu alifariki jana jioni Februar 14. Katika kipindi cha uhai wake,maisha yake ya kazi yaligubikwa na harakati nyingi za kisiasa dhidi ya mpinzani wake Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe. Morgan Tsvangirai alianzisha chama cha Movement for Democratic Change -MDC- mwaka 2000 na kuanza kutoa changamoto kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo aliyekaa madarakani muda mrefu. Kufuatia kifo hicho Bw.Tsvangirai,MDC inaelekea kugawanyika juu ya nani atakayeongoza uchaguzi hapo baadaye mwaka huu dhini ya chama tawala cha Zanu PF, ambacho kwa sasa kinaongozwa na Emmerson Mnangagwa. Bw.Tsvangirai,Ali